Browsing by Author "Philipo, Zabron T."
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Matamshi na tahajia ya istilahi mkopo za Kiingereza katika Kiswahili: Mifano kutoka istilahi za sayansi ikisiri(The University of Dar es Salaam, 2022) Philipo, Zabron T.Lengo la makala haya ni kuonesha ruwaza ya matamshi na tahajia ya Istilahi Mkopo (kuanzia sasa IM) za Kiingereza zinazoingizwa katika Kiswahili. Mtazamo wa asasi zinazohusika na uundaji istilahi kama vile Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kuhusu matamshi na tahajia ya IM unaonesha kuwa IM zenye matamshi kama yalivyo katika Kiswahili na kuwa na tahajia ya IM zenye muundo wa maandishi kama ilivyo katika Kiingereza. Data na hoja zilizowasilishwa katika makala hii zimetokana na hojaji, usaili na upitiaji nyaraka[1]. Hivyo, data hizo zinadhihirisha kuwa kuna uhalali wa kuangalia upya ruwaza ya matamshi na tahajia ya IM za Kiingereza katika Kiswahili. Makala haya yanabainisha kuwa IM ziwe na ruwaza ya matamshi kama ilivyo katika Kiingereza. Kwa mfano, - /haidrojeni/ na tahajia iwe ni ile ya muundo wa matamshi badala ya ule wa maandishi. Kwa mfano, - *. Makala yanatoa mwongozo wa matamshi na tahajia ya IM katika Kiswahili.Item Tofauti baina ya Vivumishi na Vibainishi katika Lugha ya Kiswahili(The University of Dar es Salaam, 2017) Philipo, Zabron T.Nia ya makala hii ni kuonyesha tofauti ya dhana ‘kivumishi’ na ‘kibainishi’ katika lugha ya Kiswahili. Wanaisimu wengi, kwa kutumia mtazamo wa kimapokeo, wamekuwa wakichanganya dhana hizi mbili katika lugha hii ambapo vibainishi vimekuwa vikiwekwa kwenye ‘kapu’ moja na vivumishi. Kutokana na kuwapo kwa utata huo, makala hii inazitalii dhana hizi mbili ili kujaribu kuondoa au kupunguza utata unaowakabili wanaisimu katika kuzipambanua dhana hizi katika lugha ya Kiswahili. Mbinu ya udurusu wa nyaraka ilitumika kupata data za makala hii1. Mtazamo wa kisasa katika kuainisha tofauti baina ya vivumishi na vibainishi ulitumika. Mtazamo huu unasisitiza kutumia kigezo cha kisintaksia kupambanua aina hizi za maneno kwa kuzingatia: mosi, mtawanyiko wake, pili, dhima kisarufi, na tatu, mnyambuliko wa aina hizi za maneno. Aidha, makala hii inapendekeza vigezo na namna nyingine za kuainisha vibainishi na vivumishi katika lugha ya Kiswahili.