Humanities
Permanent URI for this community
Browse
Browsing Humanities by Subject "Abdul Ali"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mabadiliko katika nyimbo za taarab na uwasilishaji wake kulingana na wakati(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2017) Khamis, Nadra SoudUtafiti huu ulilenga kuchunguza mabadililko ya nyimbo za taarab na uwasilishaji wake kulingana na wakati, ambao ulifanyika katika Mkoa wa Mjini Magharib. Jambo kubwa lililozungumziwa katika utafiti huu ni kuchunguza namna ya matukio ya kihistoria katika jamii ya Zanzibar yalivyoweza kuathiri mabadiliko ya nyimbo za taarab na uwasilishaji wake katika vipindi husika. Kama inavyoeleweka kuwa, Zanzibar imepitiwa na vipindi mbalimbali kihistoria kama vile kipindi cha utawala wa Sultan, harakati za Mapinduzi na Uhuru na pia baada ya Mapnduzi hadi sasa. Kutokana na vipindi hivi ambavyo Zanzibar imepitia, moja kwa moja vimeweza kuathiri nyimbo za taarab kwa kutungwa na kuimbwa kulingana na wakati husika., hali hii imesababishwa na kuwa, fasihi maisha yote huwasawiri yaliyomo katika jamii. Kwa hali hiyo basi, hata utanzu huu wa nyimbo za taarab umeweza kuyasawiri yale yaliyomo katika jamii katika vipindi mbalimbali ambavyo nyimbo hizi zimepitia, na kusababisha kuibuka kwa nyimbo mbali mbali katika kipindi husika. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbali mbali kama vile, kusoma majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya mahojiano na majadiliano, ambapo mbinu hizi zilitusaidia katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali zilizohusu mada ya utafiti huu. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Mwigo, ambayo inahusu namna kazi za sanaa ikiwemo fasihi, zinavyoweza kuiga au kuchota yaliyomo katika jamii katika vipindi mbali mbali. Uchambuzi wa data uliegemea katika maelezo kwa kuwa utafiti huu ni wa kitaamuli.