Matumizi ya ramsa na tanzia katika utenzi wa Al-inkishafi wa S.A Nasir (1720-1820)

dc.contributor.authorMganga, Nawaje Ali
dc.date.accessioned2020-03-20T07:05:29Z
dc.date.available2020-03-20T07:05:29Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamivu katika Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu Matumizi ya Ramsa na Tanzia katika Utenzi wa Al-Inkishafi. Tasnifu hii imelenga kuchunguza matumizi ya ramsa na tanzia, kupitia vijenzi vya kifani, matukio, sababu na kutathmini ustadi wa matumizi ya dhana hizo za ramsa na tanzia katika Utenzi wa Al-Inkishafi (1720-1820) jinsi unavyolingana na kutafautiana. Mbinu za tasnifu zimejikita katika kushughulikia maeneo yaliyofanyika utafiti yakiwa ni maktabani na maskanini katika kisiwa cha Pate nchini Kenya. Njia zilizotumika kukusanyia data ni usaili, udurusu wa maktabani, na ushuhuda wa maskanini. Uthabiti wa data pamoja na matumizi ya mkabala wa kifasili yalihusishwa na misingi ya nadharia ya Uamilifu katika kuchambua data na kuleta tija iliyotarajiwa. Hatimaye, tasnifu imebainisha namna ilivyofuata maadili ya utafiti. Utafiti wa ramsa na tanzia katika Utenzi wa Al-Inkishafi umegundua kwamba mshairi alikuwa na sababu maalumu za kutumia dhana hizo kinzani za ramsa na tanzia, zilizomsukuma kutumia vijenzi maalumu katika matukio kadhaa, yaliyotumika katika ustadi wa kufanana na kutafautiana. Hivyo, tasnifu hii ni muhimu katika taaluma ya tenzi za Kiswahili katika kuzipanua kimawanda dhana za ramsa na tanzia kutoka katika uwanja wa tamthiliya kuelekea katika uga wa ushairi wa Kiswahili kupitia Utenzi wa Al-Inkishafi. Hivyo, wahakiki na wachambuzi wa ushairi, kuanzia sasa nawashauri kuzijumuisha dhana za ramsa na tanzia katika uhakiki na uchambuzi wao, kwa yatayohusiana na haya.en_US
dc.identifier.citationMganga, N. A. (2019). Matumizi ya ramsa na tanzia katika utenzi wa Al-inkishafi wa S. A. Nasir (1720-1820) (Tasnifu ya uzamivu). Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/2246
dc.publisherThe University of Dodomaen_US
dc.subjectRamsaen_US
dc.subjectTanziaen_US
dc.subjectUtenzi wa Al-Inkishafien_US
dc.subjectUtenzi wa Al-Inkishafi (1720-1820)en_US
dc.subjectKisiwa cha Peteen_US
dc.subjectFanien_US
dc.subjectTamthiliya kiswahilien_US
dc.subjectKenyaen_US
dc.subjectUshairien_US
dc.titleMatumizi ya ramsa na tanzia katika utenzi wa Al-inkishafi wa S.A Nasir (1720-1820)en_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
NAWAJE ALI MGANGA.pdf
Size:
7.2 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections