Ufutuhi katika nyimbo za sherehe za unyago wa Wazaramo: utumizi na dhima zake kwa hadhira

dc.contributor.authorJuma, Saad
dc.date.accessioned2019-11-26T13:13:26Z
dc.date.available2019-11-26T13:13:26Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza ujitokezaji wa ufutuhi katika nyimbo za sherehe za unyago wa Wazaramo kwa kuangalia utumizi na dhima zake kwa hadhira. Dhana ya ufutuhi imefasiliwa kuwa ni hali furaha, ucheshi, kicheko au tabasamu itokanayo na vijenzi mbalimbali. Vijenzi vya ufutuhi vilivyomakinikiwa katika utafiti huu ni kejeli, vijembe, dhihaka, na balagha. Utafiti ulifanyika uwandani na maktabani ambapo data za utafiti zilikusanywa na baadaye kuchambuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya ufafanuzi wa kimaelezo. Maeneo yaliyotumika katika kukusanya data za utafiti yalikuwa ni mikoa ya Pwani, Dar es salaam na Dodoma. Uchambuzi wa data ulizingatia misingi ya nadharia ya Uhalisia ambayo ni; uhalisia kama mwelekeo, uhalisia kama mbinu ya kisanaa, na uhalisia kama mbinu ya kihakiki. Nadharia hii ilisaidia kufafanua uwiano uliopo kati ya sanaa ya uimbaji itumikayo katika sherehe za unyago wa Wazaramo na uhalisia wa matukio ya kila siku yatokanayo na mfumo wa maisha ya jamii hii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa hali ya utani, hofu na sababu za kihistoria ndizo huwafanya Wazaramo watumie tungo za kifutuhi wakati wa sherehe za unyago. Pia, matokeo yanabainisha kuwa Wazaramo hutumia ufutuhi katika nyimbo za unyago wa kama kibebeo cha fikra, na hisia zinazolengwa kuwekwa wazi mbele ya hadhira iliyokusanyika. Ufutuhi unaochopekwa katika tungo hizi huifanya hadhira kuzing'amua na kuzielewa kwa njia iliyojaa ucheshi, kicheko, na tabasamu. Dhamira hizi huweza kumhusu mwali wa Kizaramo anayefanyiwa unyago, mzazi au mlezi wake pamoja na washiriki wengine waliokusanyika katika sherehe husika.en_US
dc.identifier.citationJuma, S. (2014). Ufutuhi katika nyimbo za sherehe za unyago wa Wazaramo: utumizi na dhima zake kwa hadhira (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1835
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectUfutuhien_US
dc.subjectNyimboen_US
dc.subjectUnyagoen_US
dc.subjectWazaramoen_US
dc.subjectDhimaen_US
dc.subjectHadhiraen_US
dc.subjectShereheen_US
dc.subjectFasihi simulizien_US
dc.subjectVijembeen_US
dc.subjectDhihakaen_US
dc.subjectBalaghaen_US
dc.titleUfutuhi katika nyimbo za sherehe za unyago wa Wazaramo: utumizi na dhima zake kwa hadhiraen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
SAAD JUMA.pdf
Size:
1.26 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: