Falsafa ya waafrika na ujenzi wa mtindo wa uhalisiajabu katika riwaya ya Kiswahili

dc.contributor.authorFaustine, Stella
dc.date.accessioned2020-08-25T11:17:09Z
dc.date.available2020-08-25T11:17:09Z
dc.date.issued2017
dc.descriptionTasnifu ya Uzamivuen_US
dc.description.abstractTasnifu hii ni zao la utafiti uliofanywa unaohusu Falsafa ya Waafrika na Mchango Wake katika Ujenzi wa Mtindo wa Uhalisiajabu katika Riwaya ya Kiswahili. Utafiti uliozalisha tasnifu hii umetokana na changamoto kubwa kuwa upo ugumu wa uelewekaji wa maudhui ndani ya kazi za Fasihi zinazotumia mtindo wa uhalisiajabu. Ili kutimiza azma ya kufanyika kwa utafiti huu, malengo manne yalishughulikiwa. Nayo ni kubainisha namna Falsafa ya Waafrika ilivyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili za kihalisiajabu, kujadili namna Falsafa hiyo inavyojitokeza kama kijenzi cha mtindo wa uhalisiajabu katika riwaya teule za Kiswahili za kihalisiajabu, kuainisha mtindo ya uhalisiajabu kwa kuzingatia namna unavyojitokeza katika riwaya teule za Kiswahili za kihalisiajabu, na kufafanua mchango wa mtindo wa uhalisiajabu katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Njia zilizotumika kupata data za utafiti uliozalisha tasnifu hii ni usaili, udodosaji, udurusu wa nyaraka na ushuhudiaji. Data za utafiti huu zilitafsiriwa na kuchambuliwa kwa kutumia nadharia tete ya Uhalisiajabu. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa kusawiriwa kwa Falsafa ya Waafrika katika riwaya za Kiswahili kuna mchango mkubwa katika kuujenga mtindo wa uhalisiajabu. Aidha, imebainika pia kuwa kuna aina mbalimbali za mtindo wa uhalisiajabu katika riwaya za Kiswahili za kihalisiajabu. Nazo ni: uhalisiajabu fantasia, tarazi, fifi, wa kimajazi, na wa kisitiari. Kwa upande mwingine, matokeo ya utafiti yameonesha kuwa mtindo wa uhalisiajabu una mchango mkubwa katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili, kifasihi na kijamii. Kifasihi, mtindo huu umechangia katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili kiepistemolojia, kiujumi, na katika upanuzi wa uhuru wa waandishi katika kuandika kazi zao. Kijamii, mtindo huu umeifanya riwaya ya Kiswahili kuwa ni darasa la kujifunza maarifa ya Falsafa ya Waafrika; na pia, kama ghala la kuhifadhia amali za Waafrika. Utafiti umehitimishwa kwa kupendekeza mambo makuu mawili yafuatayo: Mosi, Serikali kuweka mikakati mathubuti ya kuhakikisha kuwa lugha na Fasihi ya Kiswahili vinapewa kipaumbele katika muktadha wa elimu na jamii kwa jumla. Pili, Usomaji wa kazi za Fasihi ufanywe kwa umakini kwa kuzingatia nadharia za uhakiki zinazoendana na kazi husika na muktadha wa jamii.en_US
dc.identifier.citationFaustine, S. (2017). Falsafa ya waafrika na ujenzi wa mtindo wa uhalisiajabu katika riwaya ya Kiswahili, (Tasnifu ya uzamivu). Chuo kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/2421
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectUhalisiajabuen_US
dc.subjectFalsafa ya waafrikaen_US
dc.subjectRiwaya ya kiswahilien_US
dc.subjectRiwayaen_US
dc.subjectUjenzi wa mtindoen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectWaafrikaen_US
dc.titleFalsafa ya waafrika na ujenzi wa mtindo wa uhalisiajabu katika riwaya ya Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
STELLA FAUSTINE.pdf
Size:
2.48 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections