Uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma: Mifano kutoka shule za msingi Tanzania

Loading...
Thumbnail Image
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The University of Dodoma
Abstract
Utafiti huu umechunguza uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania zinazotumia mchepuo wa Kiswahili, hasa kwa kujikita katika mtaala wa Kiswahili. Malengo mahususi yaliyoshughulikiwa na utafiti huu ni matatu. Malengo hayo ni kuchambua viakifishi vinavyotumiwa katika uandishi wa kitaaluma wa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania, kuchunguza makosa ya uakifishaji yanavyojitokeza katika kazi za wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania na kubainisha sababu mbalimbali za makosa ya uakifishaji kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania. Utafiti huu umetumia mbinu mseto katika kukusanya data. Vilevile, umetumia mkabala wa kiidadi na wa kitaamuli kuwasilisha na kujadili data. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba wanafunzi wa Shule za Msingi wanafundishwa na wanatumia viakifishi vichache. Viakifishi hivyo ni nukta, kiulizo, mkato na mshangao, huku vingine vikitumika mara chache. Pia, matokeo ya utafiti yameonesha kuwa wanafunzi hawawezi kuakifisha kazi zao kwa usahihi kwa sababu hawafundishwi uakifishaji kwa kina, marefu na mapana. Kwa hali hiyo, wanafunzi hao huandika sentensi bebanifu, sentensi tata na vipande sentensi. Kwa hiyo, utafiti huu unapendekeza uakifishaji kufundishwa kama mada inayojitegemea katika viwango vyote vya elimu, Shule za Msingi, Sekondari hadi Vyuo Vikuu, ili wanafunzi waweze kuzielewa sheria na kanuni za uakifishaji na hivyo kuboresha maandiko yao ya kitaaluma.
Description
Tasnifu ya uzamivu
Keywords
Uandishi wa kitaaluma, Viakifishi, Shule za msingi, Tanzania, Uzingatizi, Makosa ya uakifishaji, Uchambuzi wa viakifishi
Citation
Stephano, R. (2015). Uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma: Mifano kutoka shule za msingi Tanzania (Tasnifu ya uzamivu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.
Collections