Usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhando
Loading...
Date
2014
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Utafiti huu umejadili kuhusu Usawiri wa Mwanamke katika Tamthiliya Teule za Penina Mhando. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na hali ya kila siku ya waandishi wa tamthiliya za Kiswahili wakiwemo wanaume, kumkweza mwanaume kinafasi na kimajukumu na kumshusha mwanamke, hivyo utafiti huu ulijikita kuchunguza nafasi ya mwanamke katika tamthilia teule za Penina Muhando. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani kwa kuchunguza kazi mbalimbali ili kupata ruwaza ya jumla kuhusu nafasi ya mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia, pia vitabu teule ambavyo ni Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982) vimesomwa na kuchunguzwa kwa makini na kuona jinsi mwanamke alivyochorwa. Mahojiano yalifanyika ili kupata mawazo mbalimbali kuhusu mada ya utafiti. Pia umeongozwa na nadharia ya Ufeministi. Hivyo utafiti huu umebaini kuwa kuna tofauti kubwa za kimajukumu kati ya mwanaume na mwanamke. Kwa upande mmoja mwanamke amechorwa kwa mtazamo hasi na chanya yaani ameonekana ni kiumbe duni, mnyonge, na hivyo kuendelea kumdharau, kumkejeli na kumdhihaki. Kwa upande mwingine mwanamke amechorwa kama mshauri, mlezi, mbunifu, mvumilivu na mtu mwenye huruma na ushirikiano katika jamii. Pia utafiti huu umebaini kuwa zipo athari mbalimbali zinazosababishwa na uchorwaji wa mwanamke katika tamthilia.
Athari mojawapo ni kuigwa kwa matendo machafu ambayo yanasababisha kudharaulika na kuendelea kukandamizwa kwa wanawake. Hivyo basi kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa katika jamii nafasi ya mwanamke na mgawawanyo wa majukumu huwa tofauti na mwanaume kwa sababu ya mila na tamaduni mbovu ambazo humchukulia mwanamke kama kiumbe duni wakati wote ingawa uhalisia wa sasa hauko hivyo.
Description
Tasnifu (MA Kiswahili)
Keywords
Kiswahili, Jinsia, Hati, Nguzo mama, Majukumu, Unyonge, Mila, Tamaduni, Usawiri mwanamke, Usawiri mwanaume, Tamthiliya, Tamthiliya kiswahili, Penina Mhando, Nadharia ufeministi
Citation
George, G. (2014). Usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhando (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.