Ufanisi wa tafsiri za viwandani nchini Tanzania: uchunguzi wa vifungashio vya dawa za binadamu
Loading...
Date
2020
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Makala haya yanahusu tafsiri za vifungashio vya dawa za binadamu. Lengo kuu la kuandika makala haya lilikuwa kuchunguza ufanisi wa tafsiri za vifungashio hivyo. Methodolojia ya utafiti huu imejumuisha upitiaji wa tafsiri na usaili kwa wafamasia na watumiaji wa dawa. Lengo la kuwasaili wafamasia ni kupata taarifa kuhusu dhima ya wamiliki wa viwanda vya dawa kufanya tafsiri. Usaili wa watumiaji wa dawa ulilenga kuangalia tija za tafsiri za vifungishio vya dawa, hasa katika Kiswahili kwa watumiaji hao. Matokeo ya utafiti wetu yanaonesha kuwa ufanisi wa tafsiri hufikiwa pale tafsiri inapokidhi dhima zake. Uchunguzi wa vifungashio vya dawa umeonesha matokeo ya aina mbili ambayo ni kufanikiwa na kutofanikiwa kwa tafsiri katika dhima zake. Kufanikiwa kwa tafsiri katika vifungashio vya dawa za binadamu kumejionesha katika dhima mbalimbali kama vile kufanikisha mawasiliano, kufundisha na kujifunza lugha, pamoja na kupanua soko na kuwapa amani walaji wa bidhaa. Kutofanikiwa kwa tafsiri hizi kumetokana na kasoro kama vile udondoshaji, upotoshaji wa taarifa muhimu na kutozingatia sarufi ya lugha lengwa. Kutokana na kutofanikiwa kwa tafsiri za vifungashio hivyo vya dawa, utafiti huu unapendekeza tafsiri sahihi kuzingatiwa ili kukidhi mawasiliano pamoja na dhima nyingine za tafsiri. Kwa kufanya hivyo, dawa zitaweza kununuliwa na watu wengi zaidi kutokana na kuelewa maelekezo yanayotolewa katika lugha mbalimbali.
Description
Ikisiri. Makala kamili inapatikana https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/3158
Keywords
Vifungashio, Dawa binadamu, Tafsiri viwandani, Uchunguzi vifungashio, Utumiaji dawa, Kiswahili, Vifungashio vya dawa
Citation
Stephano, R. & Gwajekera, F. D. (2020). Ufanisi wa tafsiri za viwandani nchini Tanzania: uchunguzi wa vifungashio vya dawa za binadamu. Jarida la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, JUZ. 38 (26-42)