Ufanisi wa tafsiri za viwandani nchini Tanzania: uchunguzi wa vifungashio vya dawa za binadamu

dc.contributor.authorStephano, Rehema
dc.contributor.authorGwajekera, Fidel Dassan
dc.date.accessioned2021-08-31T09:21:04Z
dc.date.available2021-08-31T09:21:04Z
dc.date.issued2020
dc.descriptionIkisiri. Makala kamili inapatikana https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/3158en_US
dc.description.abstractMakala haya yanahusu tafsiri za vifungashio vya dawa za binadamu. Lengo kuu la kuandika makala haya lilikuwa kuchunguza ufanisi wa tafsiri za vifungashio hivyo. Methodolojia ya utafiti huu imejumuisha upitiaji wa tafsiri na usaili kwa wafamasia na watumiaji wa dawa. Lengo la kuwasaili wafamasia ni kupata taarifa kuhusu dhima ya wamiliki wa viwanda vya dawa kufanya tafsiri. Usaili wa watumiaji wa dawa ulilenga kuangalia tija za tafsiri za vifungishio vya dawa, hasa katika Kiswahili kwa watumiaji hao. Matokeo ya utafiti wetu yanaonesha kuwa ufanisi wa tafsiri hufikiwa pale tafsiri inapokidhi dhima zake. Uchunguzi wa vifungashio vya dawa umeonesha matokeo ya aina mbili ambayo ni kufanikiwa na kutofanikiwa kwa tafsiri katika dhima zake. Kufanikiwa kwa tafsiri katika vifungashio vya dawa za binadamu kumejionesha katika dhima mbalimbali kama vile kufanikisha mawasiliano, kufundisha na kujifunza lugha, pamoja na kupanua soko na kuwapa amani walaji wa bidhaa. Kutofanikiwa kwa tafsiri hizi kumetokana na kasoro kama vile udondoshaji, upotoshaji wa taarifa muhimu na kutozingatia sarufi ya lugha lengwa. Kutokana na kutofanikiwa kwa tafsiri za vifungashio hivyo vya dawa, utafiti huu unapendekeza tafsiri sahihi kuzingatiwa ili kukidhi mawasiliano pamoja na dhima nyingine za tafsiri. Kwa kufanya hivyo, dawa zitaweza kununuliwa na watu wengi zaidi kutokana na kuelewa maelekezo yanayotolewa katika lugha mbalimbali.en_US
dc.identifier.citationStephano, R. & Gwajekera, F. D. (2020). Ufanisi wa tafsiri za viwandani nchini Tanzania: uchunguzi wa vifungashio vya dawa za binadamu. Jarida la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, JUZ. 38 (26-42)en_US
dc.identifier.otherURL: https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/3158
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/3313
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dar es Salaamen_US
dc.subjectVifungashioen_US
dc.subjectDawa binadamuen_US
dc.subjectTafsiri viwandanien_US
dc.subjectUchunguzi vifungashioen_US
dc.subjectUtumiaji dawaen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectVifungashio vya dawaen_US
dc.titleUfanisi wa tafsiri za viwandani nchini Tanzania: uchunguzi wa vifungashio vya dawa za binadamuen_US
dc.typeArticleen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Stephano & Gwajekera.pdf
Size:
6.13 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections