Ukiukwaji wa nadharia tumizi ya uakifishaji katika kazi za kitaaluma za wanafunzi wa shule za msingi Tanzania
Loading...
Date
2020
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Makala haya ni zao la tasnifu ya Stephano (2015) yenye mada ya “Uzingatizi wa Viakifishi katika Uandishi wa Kitaaluma: Mifano kutoka Shule za Msingi Tanzania.” Makala inabainisha misingi mikuu ya Nadharia Tumizi ya Uakifishaji na kuonesha ukiukwaji wake katika nyaraka zinazotumika kufundishia na kujifunzia Kiswahili katika shule za msingi. Data za utafiti huu zimetokana na mapitio ya nyaraka za kufundishia na kujifunzia Kiswahili. Nyaraka hizo ni vitini vya masomo ya wanafunzi wa Darasa la VI na VII, na vitabu vya kiada na viongozi vya walimu Darasa I - VII. Matokeo ya uchunguzi wetu yanaonesha kuwa Nadharia Tumizi ya Uakifishaji haizingatiwi kwa uhakika, hasa katika uandishi wa insha. Ni viakifishi vichache tu, nukta, kiulizo, mshangao (viakifishi vya Safu 1) na mkato (kiakifishi cha Safu 4) ikilinganishwa na idadi inayopendekezwa na nadharia (ambavyo ni viakifishi kumi na vinne), ndivyo vinavyotumika. Zaidi, matokeo yanaonesha kuwa, pamoja na kutumika, viakifishi hivyo havitumiki kwa usahihi. Kwa hiyo, makosa ya kuandika sentensi bebanifu, sentensi tata na vipande sentensi hutokea. Makala yanapendekeza Nadharia Tumizi ya Uakifishaji kuzingatiwa wakati wa kuandika ili kuandika matini zinazoeleweka kwa wasomaji.
Description
Ikisiri. Makala kamili inapatikana https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/2462
Keywords
Nadharia uakifishaji, Wanafunzi shule msingi, Tumizi uakifishaji taaluma, Kiswahili, Nadharia tumizi uakifishaji matini, Shule msingi, Tanzania
Citation
Stephano, R. (2020). Ukiukwaji wa nadharia tumizi ya uakifishaji katika kazi za kitaaluma za wanafunzi wa shule za msingi Tanzania.Jarida la Taasisi la Taaluma za Kiswahili, Juz. 153(37)