Ukiukwaji wa nadharia tumizi ya uakifishaji katika kazi za kitaaluma za wanafunzi wa shule za msingi Tanzania

dc.contributor.authorStephano, Rehema
dc.date.accessioned2021-05-28T07:20:27Z
dc.date.available2021-05-28T07:20:27Z
dc.date.issued2020
dc.descriptionIkisiri. Makala kamili inapatikana https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/2462en_US
dc.description.abstractMakala haya ni zao la tasnifu ya Stephano (2015) yenye mada ya “Uzingatizi wa Viakifishi katika Uandishi wa Kitaaluma: Mifano kutoka Shule za Msingi Tanzania.” Makala inabainisha misingi mikuu ya Nadharia Tumizi ya Uakifishaji na kuonesha ukiukwaji wake katika nyaraka zinazotumika kufundishia na kujifunzia Kiswahili katika shule za msingi. Data za utafiti huu zimetokana na mapitio ya nyaraka za kufundishia na kujifunzia Kiswahili. Nyaraka hizo ni vitini vya masomo ya wanafunzi wa Darasa la VI na VII, na vitabu vya kiada na viongozi vya walimu Darasa I - VII. Matokeo ya uchunguzi wetu yanaonesha kuwa Nadharia Tumizi ya Uakifishaji haizingatiwi kwa uhakika, hasa katika uandishi wa insha. Ni viakifishi vichache tu, nukta, kiulizo, mshangao (viakifishi vya Safu 1) na mkato (kiakifishi cha Safu 4) ikilinganishwa na idadi inayopendekezwa na nadharia (ambavyo ni viakifishi kumi na vinne), ndivyo vinavyotumika. Zaidi, matokeo yanaonesha kuwa, pamoja na kutumika, viakifishi hivyo havitumiki kwa usahihi. Kwa hiyo, makosa ya kuandika sentensi bebanifu, sentensi tata na vipande sentensi hutokea. Makala yanapendekeza Nadharia Tumizi ya Uakifishaji kuzingatiwa wakati wa kuandika ili kuandika matini zinazoeleweka kwa wasomaji.en_US
dc.identifier.citationStephano, R. (2020). Ukiukwaji wa nadharia tumizi ya uakifishaji katika kazi za kitaaluma za wanafunzi wa shule za msingi Tanzania.Jarida la Taasisi la Taaluma za Kiswahili, Juz. 153(37)en_US
dc.identifier.otherURL: https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/2462
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/3257
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherTaasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaamen_US
dc.subjectNadharia uakifishajien_US
dc.subjectWanafunzi shule msingien_US
dc.subjectTumizi uakifishaji taalumaen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectNadharia tumizi uakifishaji matinien_US
dc.subjectShule msingien_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleUkiukwaji wa nadharia tumizi ya uakifishaji katika kazi za kitaaluma za wanafunzi wa shule za msingi Tanzaniaen_US
dc.typeArticleen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Stephano, Rehema.pdf
Size:
100.3 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections