Juma, Saad2019-11-262019-11-262014Juma, S. (2014). Ufutuhi katika nyimbo za sherehe za unyago wa Wazaramo: utumizi na dhima zake kwa hadhira (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.http://hdl.handle.net/20.500.12661/1835Tasnifu (MA Kiswahili)Utafiti huu ulichunguza ujitokezaji wa ufutuhi katika nyimbo za sherehe za unyago wa Wazaramo kwa kuangalia utumizi na dhima zake kwa hadhira. Dhana ya ufutuhi imefasiliwa kuwa ni hali furaha, ucheshi, kicheko au tabasamu itokanayo na vijenzi mbalimbali. Vijenzi vya ufutuhi vilivyomakinikiwa katika utafiti huu ni kejeli, vijembe, dhihaka, na balagha. Utafiti ulifanyika uwandani na maktabani ambapo data za utafiti zilikusanywa na baadaye kuchambuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya ufafanuzi wa kimaelezo. Maeneo yaliyotumika katika kukusanya data za utafiti yalikuwa ni mikoa ya Pwani, Dar es salaam na Dodoma. Uchambuzi wa data ulizingatia misingi ya nadharia ya Uhalisia ambayo ni; uhalisia kama mwelekeo, uhalisia kama mbinu ya kisanaa, na uhalisia kama mbinu ya kihakiki. Nadharia hii ilisaidia kufafanua uwiano uliopo kati ya sanaa ya uimbaji itumikayo katika sherehe za unyago wa Wazaramo na uhalisia wa matukio ya kila siku yatokanayo na mfumo wa maisha ya jamii hii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa hali ya utani, hofu na sababu za kihistoria ndizo huwafanya Wazaramo watumie tungo za kifutuhi wakati wa sherehe za unyago. Pia, matokeo yanabainisha kuwa Wazaramo hutumia ufutuhi katika nyimbo za unyago wa kama kibebeo cha fikra, na hisia zinazolengwa kuwekwa wazi mbele ya hadhira iliyokusanyika. Ufutuhi unaochopekwa katika tungo hizi huifanya hadhira kuzing'amua na kuzielewa kwa njia iliyojaa ucheshi, kicheko, na tabasamu. Dhamira hizi huweza kumhusu mwali wa Kizaramo anayefanyiwa unyago, mzazi au mlezi wake pamoja na washiriki wengine waliokusanyika katika sherehe husika.KiswUfutuhiNyimboUnyagoWazaramoDhimaHadhiraShereheFasihi simuliziVijembeDhihakaBalaghaUfutuhi katika nyimbo za sherehe za unyago wa Wazaramo: utumizi na dhima zake kwa hadhiraDissertation