Sanga, Aginiwe Nelson2019-09-052019-09-052018Sanga, A. N. (2018). Mkengeuko wa ujumi wa kiafrika katika hadithi fupi andishi za kiswahili kipindi cha utandawazi: mifano kutoka magazeti ya Habari Leo, Nipashe na Mwananchi (Shahada ya Uzamivu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.http://hdl.handle.net/20.500.12661/1722Tasnifu (Shahada ya Uzamivu katika Kiswahili)Hadithi fupi andishi za Kiswahili za sasa zimeonekana kukiuka jukumu la kuusawiri uzuri wa Kiafrika, jambo ambalo linawiana na hali ya utanzu huu kutopewa nafasi ya kutosha katika nyanja mbalimbali za kijamii kama ilivyokuwa kwa utanzu wa hadithi fupi simulizi hapa Tanzania. Hali hiyo, ikiendelea kama ilivyo kuna hatari ya utanzu huu kupotea au kumezwa na tanzu nyingine kama riwaya. Aidha, utafiti umechunguza mkengeuko wa ujumi wa Kiafrika kwa kuhusianisha na mabadiliko yanayojitokeza katika jamii ili kuonesha jinsi ilivyo muhimu kuichunguza Fasihi kwa kuihusisha na jamii inayohusika. Njia zilizotumika kukusanyia data ni mahojiano, udurusu wa maandiko na majadiliano. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Michakato ya utafiti na uchambuzi wa data iliongozwa na nadharia za Ujumi Mweusi na Umarx. Matokeo ya utafiti yanawiana na malengo ya utafiti, ambapo kutokana na ufafanuzi wa ujumi wa Kiafrika uliotolewa, inaonesha kuwa hadithi fupi andishi za Kiswahili zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na usasa pamoja na umiji. Jambo hili limesababisha utanzu huu kuibagua hadhira kirika na kimaeneo. Jamii za sasa za Kiafrika zimekengeuka kiujumi na kuvutiwa na mambo yanayofungamana na utamaduni wa Kimagharibi kuliko ya Kiafrika. Mchango mpya wa tasinifu hii ni pamoja na kuibuliwa kwa vigezo vya msingi vya uchambuzi wa ujumi wa Kiafrika katika Fasihi. Vipengele hivyo ni umoja, utu, ushababi, ukizinda, lugha, imani za dini na ushirikina, na umakusudio. Aidha, Fasihi imeonekana kuwa na umuhimu kwa jamii kuliko Fasihi yenyewe na uzuri wa Fasihi unaonekana pale inapoisaidia jamii katika utimilizaji wa majukumu mbalimbali.enUjumiHadithiHadithi fupiTanzaniaUjumi wa KiafrikaUjumi mweusiUmarxFasihiMkengeuko wa ujumi wa kiafrika katika hadithi fupi andishi za kiswahili kipindi cha utandawazi: Mifano kutoka magazeti ya Habari Leo, Nipashe na MwananchiThesis