Zahoro, Selanda2019-08-192019-08-192018Zahoro, S. (2018). Vionjo vya Fasihi ya kisasa ya Kiswahili katika nyimbo teule za Singeli (Tasnifu ya Shahada ya Umahir). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.http://hdl.handle.net/20.500.12661/859Tasnifu (Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili)Tasnifu hii inahusu vionjo vya fasihi ya kisasa ya Kiswahili katika nyimbo teule za singeli. Malengo mahususi ya utafiti yalikuwa matatu: Mosi, kufafanua misingi ya nyimbo teule za singeli. Pili, kubainisha vionjo vya fasihi ya kisasa ya Kiswahili vilivyotumiwa katika nyimbo teule za singeli. Na, tatu, kutathmini athari za vionjo vya fasihi ya kisasa ya Kiswahili vinavyojitokeza katika nyimbo teule za singeli kwa jamii. Vionjo vya kisasa vya Kiswahili ni sifa zinazotumiwa katika tanzu mbalimbali za fasihi, zikiwemo ushairi, riwaya na tamthiliya. Singeli ni aina ya muziki wenye mapigo ya haraka haraka ambao umechukua vionjo vyake kutoka katika ngoma mbalimbali za asili za kabila la Wazaramo na muziki wa taarabu. Kutokana na uhaba wa tafiti na tahakiki zilizofanywa kuhusu nyimbo za singeli, utafiti ulikusudia kuziba pengo hilo. Utafiti ulitumia usanifu wa kifani uliojiegemeza katika mkabala wa kitaamuli. Data za utafiti zilikusanywa katika mkoa wa Dar es Salaam. Mbinu zilizotumika wakati wa ukusanyaji wa data ni udurusu wa maandiko, usaili na ushuhudiaji. Nadharia ya Usasa ilitumika kufanikisha mchakato wa utafiti. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, nyimbo za singeli zimejikita katika kutoa burudani kwa jamii, kutumika kama chanzo cha ajira na kuutambulisha muziki halisi wa Kitanzania. Aidha, nyimbo za singeli zimechochea kufifia zaidi kwa ngoma za asili za Kizaramo, kuchochea ufyosi katika jamii na kuhamasisha ngono. Pia, matokeo yameonesha kuwa, ngoma mbalimbali kutoka kabila la Wazaramo pamoja na taarabu vimechangia katika kuibuka kwa muziki wa singeli.KiswFasihiNyimboSingeliTanzuMuzikiTaarabu.Dar es SalaamAjiraUfyosiWazaramoVionjo vya Fasihi ya kisasa ya Kiswahili katika nyimbo teule za SingeliDissertation