Kaponda, George John2019-08-192019-08-192018Kaponda, G. J. (2018). Ontolojia ya kiafrika katika mbolezi za wanyasa (Tasnifu shahada ya Kiswahili). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.http://hdl.handle.net/20.500.12661/858Tasnifu (Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili)Tasnifu hii inahusu Ontolojia ya Kiafrika katika Mbolezi za Wanyasa. Utafiti huu ulifanywa uwandani na maktabani ambapo uwandani, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, ushuhudiaji na mjadala wa vikundi. Kwa upande wa maktabani mtafiti alitumia mbinu ya udurusu maktaba.Utafiti uliongozwa na lengo kuu ambalo ni kubaini vipengele vya ontolojia ya Kiafrika katika mbolezi za Wanyasa. Malengo mahususi ambayo ni; kubainisha aina ya mbolezi zinazopatikana katika jamii ya Wanyasa, kubainisha vipengele vya ontolojia ya Kiafrika ya katika mbolezi za Wanyasa na kutathimini umuhimu wa ontolojia ya Kiafrika kwa jamii ya Wanyasa na Waafrika kwa ujumla. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Ontolojia, mtafiti alikusanya mbolezi na dhana mbalimbali za ontolojia ya Kiafrika katika jamii ya Wanyasa. Jumla ya watafitiwa walioshiriki ni mia moja. Katika data zilizokusanywa, vipengele vilivyojitokeza vilijenga msingi wa data kuu iliyofanyiwa uchambuzi na kujadiliwa. Matokeo yanaonesha kuwa mbolezi zimegawanyika kulingana na vigezo vya chimbuko, rika na wakati. Katika chimbuko kuna mbolezi za asili na mbolezi changamani. Katika rika kuna mbolezi za watoto na mbolezi za watu wazima. Aidha, katika wakati kuna mbolezi za mara baada ya msiba kutokea, buriani, ibada ya mazishi na mazishi. Vipengele vya ontolojia ya Kiafrika vilivyobainishwa ni Mungu, ardhi, roho, kifo, mizimu na utu. Vipengele hivi vimebainika kuwa vimejengwa kiherakia na kutegemeana katika nguvu ijulikanayo kama kani uhai. Aidha, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa jamii inaendelea kudumisha umoja na mshikamano, kurithisha amali, kulinda maadili, kutolea elimu na utambulisho wa jamii. Utafiti huu umependekeza tafiti nyingi zaidi ziendelee kufanyika kuhusiana na ontolojia ya Kiafrika katika fasihi simulizi.KiswOntolojiaMboleziUdurusuRikaMunguRohoKifoMizimuUtuAfricaUmojaMshikamano,AmaliMaadili,Fasihi simuliziWanyasaAsiliChangamaniKiherakiaKani uhaiNadhariaMsibaOntolojia ya kiafrika katika mbolezi za wanyasaDissertation