Mgunda, John Madirisha2020-03-052020-03-052014Mgunda, J. M. (2014). Dhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: Mifano kutoka kwa Wasukuma (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.http://hdl.handle.net/20.500.12661/1994Tasnifu (MA Kiswahili)Visasili ni hadithi zinazoelezea desturi, itikadi, jadi na dini ambazo watu wa kale walizifuata (kuzishika) kutokana na mafundisho yaliyotokana na masimulizi hayo, wakiwa na uwezo wa kufanya miujiza kutokana nguvu za asili. Visasili vina dhima ya kuelimisha, kuonya, kuburudisha na kuadilisha kama tanzu zingine za fasihi simulizi. Utafiti huu ulikusanya visasili na kuchambua amali za kitamaduni za jamii ya Wasukuma ambazo zinahifadhiwa na kurithishwa katika visasili hivyo. Katika kukidhi matakwa ya malengo ya utafiti huu, kiunzi cha nadharia ya Masimulizi ya Mdomo na Uasilia zilitumiwa katika kuchambua data. Data zilikusanywa katika wilaya ya Magu, Kwimba, Nyamagana na Misungwi. Mbinu ya hojaji ilitumika sambamba na maandiko mbalimbali kutoka kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dodoma na Dar es Salaam, maandiko yaliyotafiti kuhusu visasili vya jamii mbalimbali, vilevile, katika kupata wawakilishi utafiti huu ulitumia sampuli lengwa (ya kimakusudi) kwa kuzingatia sifa za watafitiwa. Utafiti huu umebaini kuwa, uhifadhi na urithishaji wa fasihi simulizi katika jamii, utaisaidia kutunza kumbukumbu za asili za jamii ya Wasukuma, kuwasaidia watafiti katika utanzu huu wa visasili na kupanua mawanda mapana ya uelewa katika jamii. Visasili kama tanzu zingine za fasihi simulizi, huonesha asili ya jamii husika hasa kupitia kwenye masimulizi na matambiko. Ni utanzu unaorejesha fikra za mwanadamu kuona namna wanadamu wa kale walivyoishi kwa kuabudu miungu waliyoiamini na kuwatatulia matatizo yao. Hakuna jamii ambayo haina historia yake na utamaduni wake, hivyo, wataalam mbalimbali wa fasihi simulizi wanapaswa kushughulika katika tafiti mbalimbali ili kupata ukweli wa kila jamii wa desturi na mila zake.KiswVisasiliHadithiDesturiFasihi simuliziAmaliWasukumaMwanzaTanzu fasihiFasihiJamii wasukumaMaguKwimbaMisungwiNyamaganaDhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: mifano kutoka kwa WasukumaDissertation