Kiloba, Leah Yusufu2020-03-052020-03-052014Kiloba, L. Y. (2014). Korasi katika tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyoni (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.http://hdl.handle.net/20.500.12661/1993Tasnifu (MA Kiswahili)Utafiti huu ulihusu Korasi katika Tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyoni. Dhana ya korasi imetumiwa ikimaanisha matendo, fikra au maneno ya kisanaa ayatoayo mtu au kikundi cha watu katika kitendo cha kisanaa kwa njia ya uimbaji, uradidi, nathari na kuambatana na vitendo. Matumizi ya mbinu hii ya korasi hayajatafitiwa wala kuhakikiwa vya kutosha katika Fasihi ya Kiswahili. Hali hii inakifanya kipengele hiki kutojulikana sana na wasomi na wanajamii wengi. Tamthiliya za waandishi teule zilizotafitiwa ni Kwenye Ukingo wa Thim, Ngoma ya Ng’wanamalundi na Mabepari wa Bongo. Utafiti huu ulifanyika maktabani kwa kiasi kikubwa. Vilevile mtafiti alifanikiwa kuzungumza na wataalamu mbalimbali wa fasihi ili kupata mawazo komavu kuhusiana na mada. Uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti uliongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji kupitia nguzo yake kuu ya uhuru wa msomaji wa kupata maana kutokana na uzoefu wake. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kipengele cha korasi hutumika katika tamthiliya kwa malengo mahususi na wala si kwa bahati nasibu tu. Mchango mpya ulioibuliwa na utafiti huu ni: Kwanza, ni kupanua ufafanuzi wa dhana ya korasi. Pili, ni kuonyesha nafasi ya korasi katika tamthiliya, hususani katika tamthiliya za waandishi teule. Tatu, ubainishaji na uchambuzi wa dhima za korasi ambazo ni kutambulisha onyesho, kuunganisha onyesho moja na jingine, kuwasilisha dhamira, kudhihirisha ujumi, kujenga taharuki, kuleta ucheshi na kufunga onyesho. Hivyo, korasi hutumika kama nguzo katika ujenzi na uendelezaji wa tamthiliya.KiswKorasiTamthiliyaKiswahiliUimbajiUradidiTamthiliya kiswahiliDhimaKwenye ukingo wa ThimNadharia mwitikoEbrahim HusseinEmmanuel MbogoFrowin NyoniNgoma Ng’wanamalundiMabepari bongoKorasi katika tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin NyoniDissertation