Browsing by Author "Hemed, Bimkubwa Abdulrahman"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Athari za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa nyimbo za watoto waishio Mijini(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2015) Hemed, Bimkubwa AbdulrahmanUtafiti huu umechunguza namna Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inavyoathiri nyimbo za watoto hususan maeneo ya mijini ambako maendeleo hayo ya sayansi na teknolojia ndiko yanakopatikana kwa wingi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Usosholojia iliyoasisiwa kwa kuja kupingana na ulimbwende karne ya kumi na tisa. Utafiti huu umejumuisha mbinu ya mahojiano na hojaji kukusanya data hatimaye imechanganuliwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano yaliyopo nchini hususan mijini, yameathiri kwa kiasi kikubwa nyimbo za watoto kutokana na kuwepo kwa vyombo vingi vya habari hapa nchini, ambao ushindani wao wa kibiashara ndio unaowafanya warushe hewani nyimbo za wasanii mbali mbali na kuacha zile za watoto ambapo watoto walikuwa wanaziimba kabla yake. Suala la msingi lililobainishwa na utafiti huu ni kwamba nyimbo za watoto zimeathiriwa na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mapendekezo yafuatayo yamezingatiwa. Serikali na jamii wafanye juhudi za makusudi kurejesha hadhi ya nyimbo za watoto kwa kuziingiza katika mitaala ya shule pamoja na wazazi kufanya juhudi za makusudi kuwafundisha nyimbo hizo ili zisiendelee kupotea. Pia, imependekezwa tafiti zaidi zifanywe kuhusu tanzu mbalimbali za fasihi simulizi, na kwamba watafiti wasikidharau kipengele hiki cha nyimbo za watoto kwani mbali na kutoa burudani, pia watoto hupata mazoezi ya kutosha nakuwafanya wawe wakakamavu na wenye afya.