Browsing by Author "Kalinga, Joyce"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahli: Ulinganisho wa Kichomi na Tungizi za Mnyagatwa(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Kalinga, JoyceTasnifu hii inahusu matumizi ya vionjo vya kisasa katika ushairi wa Kiswahili. Utafiti huu ulijikita katika kulinganisha na kulinganua vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahili katika diwani za Kichomi na Tungizi za Mnyagatwa. Vionjo katika tasnifu hii imetumika kama hali ya umajaribio au mwondoko wa utanzu wa ushairi au utanzu fulani kutoka sura iliyozoeleka kwenda sura mpya ambayo haijazoeleka. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni: kubainisha vionjo vya fasihi ya kisasa katika diwani teule, kufafanua sababu za matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika diwani teule na kulinganisha na kulinganua vionjo vya fasihi ya kisasa vilivyomo katika diwani teule. Mtafiti ameamua kuchunguza matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahili kwa sababu matumizi ya vionjo vya kisasa yamechunguzwa zaidi katika utanzu wa riwaya na tamthiliya, katika ushairi uchunguzi si toshelevu au havijafanyiwa uchunguzi wa kutosha. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbalimbali kama vile majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya mahojiano ili kupata data za utafiti wetu. Utafiti ulitumia nadharia ya usasa ambayo huamini katika kuanzisha vionjo vipya na kuendeleza utamaduni wa fasihi pendwa. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa utanzu wa ushairi wa Kiswahili umesheheni sana matumizi ya vionjo vya kisasa. Matumizi haya ya vionjo vya kisasa katika ushairi yanachangiwa na mambo mbalimbali kama vile mabadiliko ya kijamii, umajaribio, ongezeko la wasomi, maingiliano ya kiulimwengu, mahitaji ya hadhira na hata maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa. Mchango mpya wa tasinifu hii ni kuonesha vionjo vinavyotumiwa na waandishi mbalimbali katika utunzi hasa katika ushairi wa Kiswahili.