Master Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Master Dissertations by Author "Azizi, Ally"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Athari za maendeleo ya sayansi na teknolojia kwenye nyimbo za asili za Wapare(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Azizi, AllyLengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza Athari za Maendeleo ya Sayansi na Teknoilojia kwenye Nyimbo za Asili za Wapare. Mtafiti alichochewa naukweli kwamba hata kama waandishi wa fasihi simulizi, hasa nyimbo za makabilaya Kitanzania,walikuwa wamefanya kazi kubwa ya kuchambua nyimbo hizo kwa namna mbalimbali, lakini hawakuangalia na kujali uchambuzi na uchanganuzi wa athari za sayansi na teknolojia kwenye nyimbo za asili za Wapare. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Sosholojia katika uchambuzi wa data za utafiti. Msingi wa nadharia hii inaangalia uhusiano uliopo baina ya fasihi na jamii na kwamba, mabadiliko yanayotokea katika jamii ndiyo yanayosababisha kubadilika kwa fasihi na nyimbo za asili zikiwemo. Mbinu mbalimbali zilizotumika kwenye ukusanyaji wa data za utafiti huu ni usaili na ushuhudiaji, pamoja na ushiriki katika kukusanya data. Baada ya uchambuzi wa data utafiti huu uliweza kubaini kuwa, maendeleo ya sayansi na teknolojia yana athari chanya na hasi kwenye nyimbo hizo za asili za Wapare. Utafiti huu umegundua kwamba ni vigumu kuchagua faida tu za maendeleo ya sayansi na teknolojia bila ya kupata hasara zake. Utafiti ulionapia jamii ndiyo yenye jukumu la kuchagua kipi kiwepo na kipi kisiwepo katika mfumo wa maisha ya jamii husika kulingana na msukumo wa mabadiliko katika jamii. Ukweli ni kwamba hakuna chenye faida kisicho na hasara zake kwa namna yoyote ile. Utafiti huu unapendekeza kwamba ipo haja ya tafiti mbalimbali kufanyika kuhusu athari za maendeleo ya sayansi na teknolojia kwenye tanzu zingine za fasihi kama vile methali, vitendawili, na sanaa za maonyesho ili kuweza kubaini ni kwa namna gani maendeleo ya sayansi na teknolojia yameweza kuiathiri fasihi simulizi kwa undani zaidi.