Master Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Recent Submissions
Item Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka vitendawili vya Kiswahili(The University of Dodoma, 2020) Ngatungwa, Felista J.Tasnifu hii inayoitwa “Usawiri wa Falsafa ya Kiafrika katika Semi: Mifano kutoka Vitendawili vya Kiswahili” iliongozwa na malengo mahsusi matatu. Nayo ni, mosi, kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni. Pili, kujadili falsafa ya Kiafrika kama inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili na tatu, kutathmini athari ya falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Kisosholojia kupitia misingi yake kama ilivyofafanuliwa katika utafiti huu. Nadharia hii ilitumika katika michakato ya ukusanyaji wa data, uchambuzi na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti. Utafiti huu ni wa kitaamuli, umetumia usanifu wa kifenomenolojia katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Utafiti huu ulifanywa uwandani na maktabani. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, mijadala ya vikundi lengwa na udurusu wa nyaraka. Eneo la utafiti lilihusisha mikoa ya Kagera na Dodoma. Sampuli ya utafiti iligawiwa katika makundi matatu. Nayo ni wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, wanajamii wenye umri kuanzia miaka hamsini na tano na kuendelea na maandiko kuhusu vitendawili vya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika. Sampuli ilipatikana kwa kutumia mbinu ya sampuli lengwa ya mpokezo na wa kutegemeafursa. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa falsafa ya Kiafrika hudhihirika kupitia mambo mbalimbali yanayojitokeza katika maisha ya mwanadamu. Mambo hayo ni suala la umoja na ushirikiano, ndoa na uzazi, “uchawi na ushirikina”, uhai na kifo, uduara, maadili na suala la imani katika Mungu na mizimu. Aidha, kupitia mifano mbalimbali ya vitendawili vya Kiswahili, utafiti umebaini kuwa, utanzu wa vitendawili una hazina kubwa katika kuhifadhi na kutunza maarifa ya falsafa ya Kiafrika na pia falsafa hiyo ina athari kubwa katika maisha ya jamii ya Kiafrika. Utafiti umependekeza kuwa bado kuna haja ya tafiti nyingi zaidi kufanyika katika uga wa fasihi simulizi, ili kubaini ni kwa namna gani tanzu za fasihi hiyo zinaweza kutumika kama darasa la kufunza na kuhifadhi maarifa ya kifalsafa ya jamii za Waafrika.Item Demonstrative pronouns in Cigogo language: morphology, semantics and pragmatics(The University of Dodoma, 2021) Kuta, Edward ElishaThis study is a result of an investigation done in order to describe the Cigogo language demonstratives in terms of morphology, semantics and pragmatics. The force behind conducting this study is to contribute to the theory of demonstratives by analyzing the Cigogo language demonstratives and recording them so as they can be used as an important record for language knowledge and research purposes. This is in order to maintain the stability of this ethnic community language. The study employed descriptive research design where data was collected through questionnaires, observation and structured interview and Informants were obtained through simple random sampling technique in sampling exercise. The study was guided by the following four objectives which were: to identify demonstrative pronouns in Cigogo language, to describe the morphology of Cigogo demonstrative pronoun, to describe the semantics of Cigogo demonstrative pronouns and to describe the pragmatic of use of Cigogo demonstrative pronouns. The theoretical and empirical literature was surveyed in order to have a clue of what others have found in relation to the study. The data collected by questionnaire were thematically analyzed, ELAN were used for transcription of sound and video data and texts were analyzed by using soft ware for transcription and SIL Field work explorer for creating text for data base and performing morphological analysis (annotation) and creating concordances for interview and focused group discussion. The findings of the study reveals that the Cigogo demonstrative pronouns are formed in four ways which are:-(i)by reduplication of pronominal prefix,(ii) by reduplication of pronominal prefix + affix -na, (iii)by reduplication of pronominal prefix+ affix-o, and (iv) by reduplication of pronominal prefix + affix -lya.The study provides two kinds of recommendations which are recommendation for action and recommendations for further study. That there are other aspects of this language to be reviewed and analysed in order to make the language stable with enough data for record and learning. So many other studies should be conducted to stabilize this language in all aspects. Also the study suggests that governmental and non-governmentals take holders should take serious measures to the stipulated weaknesses in measures taken to preserve our vernacular languages by ensuring our culture is promoted so as to activate positive attitude of vernacular language speakers towards their language, which will be possible by documentation of all aspects of cultural materials and writing grammar such as Morphology and Semantic books, to enable the learning of the languages to native and non native speakers.Item The structure of Chasu noun phrase(The University of Dodoma, 2020) Ndimangwa, Elihazin ChristopherThis study sought to provide a critical analysis of the Structure of Chasu Noun Phrase (NP), specifically, the southern Chasu dialect spoken in Same District of Kilimanjaro Region. The study paid attention on the morph-syntactic properties of Chasu NP, the order of elements of the NP, and constraints which determine the recurrence and co-occurrence of the NP elements. Using qualitative techniques compounded by the descriptive design, data were collected through elicitation, text collection, and direct observations. Introspection was used to supplement information drawing from the researcher’s own experience as a native speaker of Chasu. The X bar Theory of Phrase Structure by Noam Chomsky (1970), and further developed by Jackendoff (1977) was used to inform the research, particularly on the internal categories of the NP. Thematic analysis was employed to analyse the data and, thereafter, followed by thick descriptions and discussions. The findings revealed that Chasu NP constitute head with or without dependents. The dependents attested are possessive, demonstrative, distributives, adjectives, associative relatives, quantifiers, numerals, and specifiers. Morover there are intensifiers which modifying adjectives in NP structure. The possessive, and distributives occupy fixed position in the NP order. Distributives occur before the head, and possessive is always placed immediately after the head. Other dependents are flexible, though in complex NP. Other elements can co-occur, except for the distributives and other determiner elements, such as demonstratives and possessives. On the other hand, distributives restrict co-occurrence with general quantifiers. This study calls for a descriptive and comparative study on NP of other undescribed Bantu languages.Item Mdhihiriko wa utanzia katika ushairi wa Kiswahili: Mifano kutoka Kichomi na Dhifa(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Machimu, JosephineTasinifu hii ilijikita katika kujadili mdhihiriko wa utanzia katika ushairi wa Kiswahili. Diwani zilizochunguzwa ni Kichomi na Dhifa. Dhana ya utanzia katika tasinifu hii imetumika kama mbinu bunilizi inayotumia vipengele mbalimbali vizuavyo huzuni, masikitiko, machungu, majonzi pamoja na maumivu ya mwili, roho na akili kwa hadhira. Utafiti umeongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni: kubainisha matukio ya utanzia yaliyodhihirika katika diwani teule, kufafanua dhima za matumizi ya utanzia katika diwani teule na kufafanua athari za matumizi ya mbinu ya utanzia kwa wasomaji kupitia diwani teule. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Data ambazo zimetupatia majibu ya tasinifu hii zilikusanywa toka kwa wataalamu wa fasihi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa njia mbili, usaili na uchanganuzi matini. Matokeo yaliyopatikana ni: kubainika kwa matukio ya utanzia katika diwani teule. Matukio hayo ni: hali ngumu ya maisha, ulemavu wa viungo, vifungo, maradhi, ukatili, majanga na vifo. Vilevile, tumebainisha dhima za matumizi ya utanzia katika kazi za fasihi. Dhima hizo ni: hujenga hisia za woga, hufikirisha, hujenga uhalisia wa maisha na kuibusha majonzi kwa hadhira lengwa. Utanzia kama mbinu ya utunzi huwa na athari hasi au chanya katika matumizi yake katika fasihi ya Kiswahili. Athari chanya ni pamoja na: kufikisha ujumbe, kuakisi uhalisia wa maisha, kuweka karibu msomaji na mwandishi na kuitafakarisha hadhira. Athari hasi ni: kupunguza wasomaji, ugumu katika kueleweka na huwapa wasomaji hali ya kukata tamaa kuhusu maisha. Kupitia tasinifu hii, wasomaji na wahakiki wataweza kufahamu sababu za waandishi kutumia utanzia katika kazi zao za kiutunzi. Halikadhalika, imeonesha namna mbinu hii inavyoweza kutumika katika kujenga maudhui, hasa katika utanzu wa ushairi. Zaidi, tasinifu imebainisha kwamba mbinu ya utanzia inaweza kutumiwa na washairi katika kujenga maudhui yao, tofauti na hapo mwanzo ambapo utanzia ulizoeleka kuonekana kwenye tamthiliya pekee.Item Usawiri wa jinsi ya kiume katika riwaya teule za Shafi Adam Shafi(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Bayyo, Festo BangaTasinifu hii inahusiana na usawiri wa jinsi ya kiume katika riwaya teule za Shafi Adam Shafi. Tasinifu hii imejengwa na malengo matatu yafuatayo: kubainisha namna jinsi ya kiume ilivyosawiriwa katika riwaya za Shafi Adam Shafi. Pia, kubainisha changamoto zinazoikabili jinsi ya kiume katika riwaya za Shafi Adam Shafi. Lengo la tatu, ni kuelezea mbinu zilizotumiwa na jinsi ya kiume katika kukabiliana na changamoto hizo. Matokeo ya utafiti uliofanyika yametolewa kwa kuzingatia malengo na maswali ya utafiti kwa kuongozwa na nadharia ya uhalisia. Kuhusu lengo la kwanza, utafiti umebaini kuwa, jinsi ya kiume inasawiriwa kama jinsi yenye ujasiri, uvumilivu, msimamo, uongozi, wanamapinduzi na katili. Kuhusu lengo la pili, utafiti umebaini kuwa, umebainisha changamoto kama: kukosa elimu, hali ngumu ya maisha, usaliti, kukosa haki na kutenganishwa na familia. Kuhusu lengo la tatu, utafiti umebaini kuwa, mbinu kama: kutafuta burudani, kushirikiana, kudai haki zao (migomo) na kutoroka shida; ni baadhi ya mbinu zinazotumiwa na jinsi ya kiume kukabiliana na changamoto husika. Kukamilika kwa tasinifu hii kumetoa mchango mpya katika uwanja wa fasihi ya Kiswahili. Kwanza, kuipa jinsi ya kiume nafasi ya kutazamwa kama ambavyo jinsi ya kike inatazamwa. Pia, kubainisha changamoto zinazoikabili jinsi ya kiume katika kuhakikisha wanafikia malengo yao. Tatu, tasinifu hii imetoa mwanga katika masuala yanayohusiana na masuala ya jinsi katika fasihi ya Kiswahili.Item Matumizi ya wakaa katika usimulizi wa riwaya za Kiswahili: Mifano kutoka Nagona na Mzingile(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Kinga, Jasmin AllyTasnifu hii inahusu wakaa katika usimulizi wa riwaya teule za Kiswahili za Nagona na Mzingile zilizotungwa na Euphrase Kezilahabi. Wakaa ni kipengele cha kifani ambacho watunzi wa kazi za kifasihi hukitumia katika kusana kazi zao. Dhana ya wakaa tumeitumia tukimaanisha muda ambao hutumika kutendeka kwa tukio fulani. Dhana hii katika riwaya ya Kiswahili haijachunguzwa vya kutosha; yumkini, hali hii inasababisha kutojulikana miongoni mwa hadhira ya kazi za fasihi. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani (katika miji ya Dodoma na Dar es Salaam). Mbinu ya ufafanuzi ndiyo imetumika kutolea matokeo ya utafiti huu. Nadharia ya naratolojia ilitumika kutokana na mihimili yake kufaa katika kubainisha ruwaza za wakaa, kuchambua misingi iliyomuongoza mtunzi kujenga wakaa katika riwaya teule na kutathmini nafasi ya wakaa katika uelewekaji wa riwaya teule. Tumepata matokeo kwa malengo yote matatu ya utafiti. Katika lengo la kwanza, utafiti umebaini kuwa, wakaa ni mbinu ya kifani inayojitokeza katika kazi za fasihi kwa kutaja ruwaza zake kama vile saa, dakika, mwaka na karne kwa lengo la kwanza. Katika lengo la pili, utafiti umebaini kuwapo kwa misingi ya wakaa kielimu, kijiografia na kiutamaduni. Kielimu, tuna misingi kama ubunifu, utangamano na watunzi wengine, falsafa na upokezi wa hadhira. Kijiografia, kuna msingi wa mazingira. Kiutamaduni, kuna misingi ya dini, mila na desturi. Kuhusu lengo la tatu, utafiti umebaini nafasi ya wakaa katika riwaya kwa jicho la kifani na kwa jicho la kimaudhui. Kifani, tumeangalia udhanaishi na kupeleka matukio mbele. Kimaudhui, tumeeleza namna wakaa unavyotafakarisha wasomaji, kutambulisha wazo rasmi na kubaini uhalisi wa kazi. Mchango mpya ulioibuliwa na tasnifu hii ni kubainisha ruwaza za wakaa kwa wasomaji pamoja na fikra zake. Utafiti umependekeza tafiti zaidi zifanyike juu ya falsafa ya wakaa katika ushairi na tamthiliya pamoja na tanzu za fasihi nenwa.Item Ubantuishaji wa kimofolojia katika vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Hakimu, JohariPamoja na kwamba lugha ya Kiswahili ina maneno mengi yaliyokopwa katika lugha ya Kiarabu, haijawa wazi ni kwa namna gani maneno hayo (hasa vitenzi) ya Kiswahili yenye asili ya Kiarabu yamepata sifa za Kibantu. Kwa hiyo, kuna masuala kadhaa kuhusu ubantuishaji wa vitenzi vya mkopo ambayo hayajawa wazi. Masuala hayo ni kama vile ubainishaji wa maumbo ya vitenzi, ufafanuzi wa michakato ya kimofolojia inayopitiwa katika ubantuishaji wa vitenzi hivyo, na tathmini ya mwelekeo wa ubantuishaji wa vitenzi hivyo. Utafiti ulifanyika katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo ulihusisha maeneo ya Tanzania bara na Zanzibar. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa njia tatu ambazo ni: upitiaji wa nyaraka, usaili na upimaji wa usahihi wa kisarufi. Katika uchanganuzi na ufasiri wa data, Nadharia ya Mofolojia Leksika na Nadharia ya Usarufishaji zilitumika. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, msambao wa vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu katika ruwaza ya vitenzi vya Kibantu unachukua maumbo kumi (10) kati ya kumi na moja (11) ya ruwaza hiyo sawa na vitenzi vya Kiswahili asilia. Tofauti kubwa ya vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu imebainika katika baadhi ya michakato ya ubantuishaji ya vitenzi hivyo. Vilevile, viambishi vya vitenzi vimechanganuliwa katika darajia nne zenye kuakisi michakato ya unyambuzi au uambatizi wa viambishi husika. Darajia hizi pia zinaakisi viwango vya ukale wa viambishi vya Kiswahili. Ukale huo umepimwa kwa enzi za kabla ya Kiswahili kukutana na Kiarabu. Baadhi ya viambishi visivyojitokeza katika vitenzi vyenye asili ya Kiarabu ni vyenye ukale wa zamani zaidi, na kwamba michakato yake kimofolojia na kifonolojia ilishakoma kabla Kiarabu kukutana na Kiswahili. Pia, vitenzi vilivyochanganuliwa kimofolojia, mwelekeo wake wa ubantuishaji umebainika kwa kutumia Nadharia ya Usarufishaji. Kutokana na nadharia hiyo, ukamilifu na usiukamilifu wa ubantuinshaji wa vitenzi hivyo umebainishwa. Ukamilifu na usiukamilifu umebainika kutokana na matumizi ya ruwaza ya vitenzi vya Kibantu na michakato ya ubantuishaji. Kwa kuwa utafiti huu umechunguza vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu, tafiti zijazo zinaweza kuchunguza aina nyingine za maneno. Hata hivyo, kwa kuwa usarufishaji hufanyika taratibu halikutolewa hitimisho la kuonesha ubantuishaji wa vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu unapokomea.Item Matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahli: Ulinganisho wa Kichomi na Tungizi za Mnyagatwa(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Kalinga, JoyceTasnifu hii inahusu matumizi ya vionjo vya kisasa katika ushairi wa Kiswahili. Utafiti huu ulijikita katika kulinganisha na kulinganua vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahili katika diwani za Kichomi na Tungizi za Mnyagatwa. Vionjo katika tasnifu hii imetumika kama hali ya umajaribio au mwondoko wa utanzu wa ushairi au utanzu fulani kutoka sura iliyozoeleka kwenda sura mpya ambayo haijazoeleka. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni: kubainisha vionjo vya fasihi ya kisasa katika diwani teule, kufafanua sababu za matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika diwani teule na kulinganisha na kulinganua vionjo vya fasihi ya kisasa vilivyomo katika diwani teule. Mtafiti ameamua kuchunguza matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahili kwa sababu matumizi ya vionjo vya kisasa yamechunguzwa zaidi katika utanzu wa riwaya na tamthiliya, katika ushairi uchunguzi si toshelevu au havijafanyiwa uchunguzi wa kutosha. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbalimbali kama vile majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya mahojiano ili kupata data za utafiti wetu. Utafiti ulitumia nadharia ya usasa ambayo huamini katika kuanzisha vionjo vipya na kuendeleza utamaduni wa fasihi pendwa. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa utanzu wa ushairi wa Kiswahili umesheheni sana matumizi ya vionjo vya kisasa. Matumizi haya ya vionjo vya kisasa katika ushairi yanachangiwa na mambo mbalimbali kama vile mabadiliko ya kijamii, umajaribio, ongezeko la wasomi, maingiliano ya kiulimwengu, mahitaji ya hadhira na hata maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa. Mchango mpya wa tasinifu hii ni kuonesha vionjo vinavyotumiwa na waandishi mbalimbali katika utunzi hasa katika ushairi wa Kiswahili.Item Dhima ya Taswira katika Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya: Mifano kutoka kwa Nasibu Abdul na Mrisho Mpoto(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Mgalula, SarahTasinifu hii ni matokeo ya utafiti uliochunguza Dhima ya Taswira katika Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya: Mifano kutoka kwa Nasibu Abdul (Diamond Platinum) na Mrisho Mpoto (Mjomba). Utafiti huu uliongozwa na malengo matatu mahsusi ambayo ni kubainisha taswira zinazojitokeza katika nyimbo za waimbaji teule, kujadili dhima ya taswira katika nyimbo za waimbaji teule na kutathmini athari za taswira katika nyimbo za waimbaji teule. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni semiotiki kupitia misingi miwili kama ilivyofafanuliwa katika utafiti huu. Utafiti ulifanyika uwandani na maktabani. Eneo la utafiti lilihusisha mkoa wa Dodoma na Dar es salaam. Data zilikusanywa kwa njia ya uchunguzi matini na usaili ambapo sampuli ilijumuisha vijana wenye umri kati ya miaka 17 hadi 35, madijei na wanafunzi wa shahada ya kwanza katika fasihi ya kiswahili. Aidha, matini zilizochunguzwa zilihusisha nyimbo za wasanii teule ambazo kwazo taswira zilibainishwa. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa, nyimbo za waimbaji teule zimesheheni matumizi ya taswira, hivyo, kuwezesha kubainishwa kwa taswira zilizojitokeza katika nyimbo teule. Miongoni mwa taswira zinazojitokeza ni pamoja na jongoo, ngongoti, roboti, chumvi, samaki, fisi, kibakuli cha vumba, ngalawa, mwiba, kuku, chui, roho, nzi, kuni, ugali, nyumba na vyumba. Aidha, dhima tulizozibaini ni pamoja na kukwepa udhibiti, kufikisha ujumbe, kuonesha ufundi wa msanii, kuvutia hadhira, kuburudisha hadhira, na kupamba kazi ya msanii. Pia, athari chanya za matumizi ya taswira ni kuibua hisia za hadhira, hukuza udadisi wa hadhira, kukua kwa kipera husika, hufanya maudhui yaeleweka kwa urahisi na kudumisha maadili ya jamii. Na athari hasi ni pamoja na kusababisha ugumu katika kupata undani wa maudhui yanayokusudiwa, kuchochea mmomonyoko wa maadili na pia kusababisha utata wa maana. Mchango mpya wa tasinifu hii ni kuonesha dhima ya matumizi ya taswira katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya kama mbinu mojawapo ya utunzi wa kazi za kifasihi. Aidha, utafiti umependekeza tafiti nyingi zaidi ziendelee kufanyika katika eneo hili la taswira katika muziki wa kizazi kipya ili kuisheheneza zaidi fasihi simulizi ya Kiswahili.Item Matumizi ya sadfa katika riwaya pendwa ya Kiswahili: Mifano kutoka Kivuli, Kikosi cha kisasi na Hofu(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Maffa, Eliamini MarkTasinifu hii ilijikita katika kujadili matumizi ya sadfa katika riwaya pendwa za Kiswahili. Sadfa ni hali ya utukiaji wa matukio kwa wakati mmoja, aghalabu kwa namna inayoshangaza au inayoashiria bahati (Wamitila, 2003). Utumiaji wa mbinu hii katika kuibua matukio husababisha riwaya, hususani riwaya pendwa, kuonekana kuwa na matukio yasiyokuwa na mantiki katika utokeaji wake. Utafiti huu ulifanyika ili kubainisha athari za matumizi ya sadfa katika riwaya pendwa kwa kuchunguza vijenzi na miktadha ya utokeaji wake katika riwaya. Riwaya teule zilizotumika kuchunguza athari za matumizi ya sadfa ni Kivuli, Hofu na Kikosi cha Kisasi. Data zilikusanywa kwa njia ya uchanganuzi matini na usaili kwa wataalamu wa fasihi. Maeneo yaliyohusika kukusanyia data ni Dodoma na Dar es Salaam. Mbinu ya usimulizi ndio iliyotumika katika uchanganuzi wa data kwa kuzingatia misingi ya nadharia ya Umuundo. Matokeo yanaonesha kuwa kuna matumizi makubwa ya sadfa katika riwaya pendwa za Kiswahili na tanzu nyingine za fasihi. Yanabainisha mandhari, mwonekano, kazi, ushujaa na muundo wa wahusika kuwa ni vijenzi vinavyochagiza kuwepo kwa sadfa katika riwaya. Aidha, matokeo yanabainisha miktadha kama: mapenzi, upelelezi, safari, hali ya kukata tamaa na kushangaza kuwa inajengwa zaidi na sadfa katika kukamilisha masimulizi. Vilevile, athari zitokanazo na matumizi ya sadfa ni: kukuza taharuki, kupeleka matukio mbele (haraka zaidi), kuwakutanisha wahusika, kuburudisha na kijenzi cha unusura. Upekee wa tasinifu hii unatokana na kuongeza mawanda ya kuzitazama riwaya pendwa kwa jicho la sadfa ili kubainisha muundo na mtindo wake. Pia, kuondoa mtazamo hasi juu ya ujenzi wa matukio katika riwaya pendwa (mtazamo unaoamini kuwa matukio ya riwaya pendwa yamejengwa katika hali isiyokuwa na mantiki). Utumikaji mzuri wa mbinu ya sadfa hufanya kazi za fasihi kuaminika kwa urahisi zaidi na hadhira lengwa.Item The presidency and challenges of shifting foreign policy and diplomatic relations in Tanzania(The University of Dodoma, 2020) Khamis, Sadifa JumaThis dissertation reports the findings of the investigation of the presidency and the challenges of shifting foreign policy and diplomatic relations in Tanzania. In particular, the study sought to establish the reasons for and implications of shifting foreign policy approach and diplomatic relations in Tanzania. The study employed qualitative research approach, through documentary reviews and interviews with key informants. The informants of the study included retired presidents, retired prime ministers, retired ministers for Foreign Affairs and officials in the Ministry of Foreign Affairs, and Foreign Policy and diplomatic relations experts from University of Dar es Salaam and University of Dodoma. Data were subjected through Qualitative Content Analysis Approach. The analysis revealed that, historically and consistently, Tanzania‘s Foreign Policy and diplomatic engagement attitudes are organized along three related but distinct value dimensions, namely cooperative, proactive and nonaligned diplomacy. Most of the conduct of the country‘s traditional foreign policy is entirely focused on the principles, which enabled the country to be predictable in its position on foreign policy issues. There are substantial changes in foreign policy orientation and approach to diplomatic relations. The country has shifted its approach to foreign policy and diplomatic relations from political and principled foreign policy and diplomatic relations to economic and pragmatic foreign policy and diplomatic relations. Consequently, economic diplomacy has become apolitical, politically unideological, and unprincipled while the economic objectives have become the driving force of Tanzania diplomacy. Tanzania‘s proactive role in international politics has declined because of less principled foreign policy and approach to diplomatic relations. There is also a strong belief in the internal economic capacity of the country; hence, the country has reduced emphasis on external influences and jeopardized the traditional position and status in international affairs. The lack of regular exposure to and engagement in strategic international debates has made the country create a vacuum of influential diplomats who could play a great role in advancing the country‘s national foreign policy and interests. The country is also sliding away from a world map and its traditional position as a champion of human rights, dignity, freedom, and economic justice.Item Investigation on the applicability of communicative approach in teaching English language in primary schools in Tanzania(The University of Dodoma, 2020) Lameck, Victor EusabyThe study aimed to investigate the applicability of the communicative approach (CA) in teaching English language in primary schools in Tanzania. Particularly, the study investigated the attitudes of the primary school English language teachers toward the CA, the adherence to the CA’s principles by the English language teachers and the involvement of the pupils in performing various communicative activities. The research was done in two districts of Kagera Region namely Bukoba Rural and Missenyi Districts. The study employed the qualitative approach whereby two instruments of data collection were used i.e. interview and observation. A total of sixty-eight (68) respondents were involved in this study. These included thirty-two (32) English language teachers and thirty-six (36) pupils. All of them were selected purposefully and interviewed. Also, the observation was conducted in the classroom during the English lessons. The findings of this study were analysed thematically and revealed that many English language teachers in primary schools had positive attitude towards the CA. It was discovered that there were very few teachers who had neutral attitude. Although English language teachers were found out to have a positive attitude, the study discovered that those teachers were not fully adhering to the CA’s principles when teaching English language. Furthermore, the findings revealed that many pupils were not actively or fully participating in performing communicative activities that they were assigned by their English language teachers in the classroom during the lessons. Basing on what was found out by this study, it is here recommended that English language teachers in primary schools be redirected to adhere to the principles of CA. Also, the government should provide regular training to the English language teachers.Item The impact of great lakes armed conflicts on security to local communities: The case of Kasulu district in Kigoma region(The University of Dodoma, 2017) Luambano, Israel DietrichThis study was designed to examine the impact of the armed conflicts in Great Lakes Region on security to local communities of Kasulu in Kigoma Region, Tanzania. The purpose of the study was to study the nature of the great lakes region conflict, its effects to the local communities in Tanzania, and the capacity challenges among the conflict stakeholders in addressing the problem in the region. This study was carried out in Kasulu District, Kigoma Region in the villages of Manyovu, Nyarubanda, Bisale and Mkongolo. A descriptive research technique was employed in this study in order to get hold of the status of the problem, effects and the strategies in place towards addressing it. Both random and purposive sampling designs were used to get a sample size of 100 respondents. Data from primary sources were gathered using questionnaires, focus group discussions and interviews. Both qualitative and quantitative instruments were employed to analyze the field data. Generally, the findings from the study revealed that despite the presence of various measures that have been taken to address the phenomenon, there are still several problems on security matters that are due to the ongoing armed conflicts in the Great Lakes Region. Given the situation above, the study concludes that persistence of armed conflicts in the Great Lake Region poses a security dilemma that lead to massive impacts to the respective countries especially local communities like in the study area. The study, therefore, recommends that local and international actors should put together their efforts in search for a sustainable solution to the problem. This is important in order to avoid more problems that would affect peoples‟ lives and their properties: being forced to leave their farms with the fear created by the illegal immigrants, hunger and famine to some households, and lives of innocent people in the study areaItem Ufasihi katika Kasida za Madrasa(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Mganga, Nawaje AliHuu ni utafiti uliofanywa juu ya ufasihi katika kasida za madrasa kutoka wilaya ya Mjini Zanzibar kwa mwaka 2013. Tafiti mbalimbali zimefanyika kabla ya utafiti huu, lakini zote hizo zimeelezea maana ya kasida, historia na dhima ya jumla ya kasida ambayo ni kumsifu mtume Muhammad (s.a.w) mfanoSimiyu (2011:89)naMulokozi (2011:14). Dhana hiyo pia imeelezwakablana BAKIZA (2010:147),Paden (2009), Tuzin (2009),Al-Mubarakpuri (2004:310), Ntarangwi (2004:67) naMulokozi (1996:70).Kwa kuchunguza kwa undani tafiti hizi zote hazijaelezea ufasihi unaojitokeza katika kasida za madrasa. Madhumuni ya utafiti huu ni kuchunguza ufasihi unaojitokeza katika kasida za madrasa. Kama wasemavyo BAKIZA (2010:82) kuwa fasihi ni sanaa ya lugha. Hivyo usanii wa kasida ni mbinu mbali mbali zilizotumika katika kasida za madrasa zenye kudhihirisha ufundi au usaniiwa lugha. Kwa mfano matumizi ya lugha, ujenzi wa muundo, uteuzi wa mtindo na uibuaji wa dhamira. Utafiti huu ni muhimu katika taaluma ya fasihi simulizi hasa katika vipengele vya fani na maudhui pamoja na kubainisha utendaji wa kasida za madrasa za wilaya ya Mjini Zanzibar.Utafiti huu utawafaa wanazuoni wengine wanaotaka kufanya utafiti zaidi kuhusu kasida. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa kianzio kwa yale masuala ambayo hajashughulikiwa katika utafiti huu. Mbinu shirikishi (kuangalia), mahojiano ya ana kwa ana na dodoso la maswali zilitumika katika kukusanya data za utafiti huu. Hatimaye nadharia ya Ujumi wa Kinudhuma ilitumika wakati wa kuwasilisha na kufafanua data za utafiti huu.Item Dhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: mifano kutoka kwa Wasukuma(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Mgunda, John MadirishaVisasili ni hadithi zinazoelezea desturi, itikadi, jadi na dini ambazo watu wa kale walizifuata (kuzishika) kutokana na mafundisho yaliyotokana na masimulizi hayo, wakiwa na uwezo wa kufanya miujiza kutokana nguvu za asili. Visasili vina dhima ya kuelimisha, kuonya, kuburudisha na kuadilisha kama tanzu zingine za fasihi simulizi. Utafiti huu ulikusanya visasili na kuchambua amali za kitamaduni za jamii ya Wasukuma ambazo zinahifadhiwa na kurithishwa katika visasili hivyo. Katika kukidhi matakwa ya malengo ya utafiti huu, kiunzi cha nadharia ya Masimulizi ya Mdomo na Uasilia zilitumiwa katika kuchambua data. Data zilikusanywa katika wilaya ya Magu, Kwimba, Nyamagana na Misungwi. Mbinu ya hojaji ilitumika sambamba na maandiko mbalimbali kutoka kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dodoma na Dar es Salaam, maandiko yaliyotafiti kuhusu visasili vya jamii mbalimbali, vilevile, katika kupata wawakilishi utafiti huu ulitumia sampuli lengwa (ya kimakusudi) kwa kuzingatia sifa za watafitiwa. Utafiti huu umebaini kuwa, uhifadhi na urithishaji wa fasihi simulizi katika jamii, utaisaidia kutunza kumbukumbu za asili za jamii ya Wasukuma, kuwasaidia watafiti katika utanzu huu wa visasili na kupanua mawanda mapana ya uelewa katika jamii. Visasili kama tanzu zingine za fasihi simulizi, huonesha asili ya jamii husika hasa kupitia kwenye masimulizi na matambiko. Ni utanzu unaorejesha fikra za mwanadamu kuona namna wanadamu wa kale walivyoishi kwa kuabudu miungu waliyoiamini na kuwatatulia matatizo yao. Hakuna jamii ambayo haina historia yake na utamaduni wake, hivyo, wataalam mbalimbali wa fasihi simulizi wanapaswa kushughulika katika tafiti mbalimbali ili kupata ukweli wa kila jamii wa desturi na mila zake.Item Korasi katika tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyoni(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Kiloba, Leah YusufuUtafiti huu ulihusu Korasi katika Tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyoni. Dhana ya korasi imetumiwa ikimaanisha matendo, fikra au maneno ya kisanaa ayatoayo mtu au kikundi cha watu katika kitendo cha kisanaa kwa njia ya uimbaji, uradidi, nathari na kuambatana na vitendo. Matumizi ya mbinu hii ya korasi hayajatafitiwa wala kuhakikiwa vya kutosha katika Fasihi ya Kiswahili. Hali hii inakifanya kipengele hiki kutojulikana sana na wasomi na wanajamii wengi. Tamthiliya za waandishi teule zilizotafitiwa ni Kwenye Ukingo wa Thim, Ngoma ya Ng’wanamalundi na Mabepari wa Bongo. Utafiti huu ulifanyika maktabani kwa kiasi kikubwa. Vilevile mtafiti alifanikiwa kuzungumza na wataalamu mbalimbali wa fasihi ili kupata mawazo komavu kuhusiana na mada. Uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti uliongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji kupitia nguzo yake kuu ya uhuru wa msomaji wa kupata maana kutokana na uzoefu wake. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kipengele cha korasi hutumika katika tamthiliya kwa malengo mahususi na wala si kwa bahati nasibu tu. Mchango mpya ulioibuliwa na utafiti huu ni: Kwanza, ni kupanua ufafanuzi wa dhana ya korasi. Pili, ni kuonyesha nafasi ya korasi katika tamthiliya, hususani katika tamthiliya za waandishi teule. Tatu, ubainishaji na uchambuzi wa dhima za korasi ambazo ni kutambulisha onyesho, kuunganisha onyesho moja na jingine, kuwasilisha dhamira, kudhihirisha ujumi, kujenga taharuki, kuleta ucheshi na kufunga onyesho. Hivyo, korasi hutumika kama nguzo katika ujenzi na uendelezaji wa tamthiliya.Item Matumizi na dhima ya uwili katika tamthiliya za kiswahili: Mifano kutoka katika tamthiliya teule za Penina Muhando (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Stephen, JeremiahTasnifu hii inahusu Uwili katika Tamthiliya za Kiswahili kwa kuangalia Tamthiliya teule za Penina Muhando. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kuchambua tamthiliya teule za Penina Muhando ili kubainisha matumizi ya uwili katika tamthiliya hizo, kueleza sababu zilizomfanya Penina Muhando kutumia mbinu za uwili katika utunzi wa tamthiliya teule, kadhalika kueleza dhima ya uwili katika tamthiliya teule za Penina Muhando. Katika utafiti huu, data zilikusanywa uwandani na maktabani. Baada ya hapo mtafiti alitumia mkabala wa maelezo katika kuchanganua data huku akiongozwa na nadharia ya Ujumi Mweusi. Utafiti huu ulibaini kuwa katika tamthiliya teule za Penina Muhando kuna uwili, yaani tamthiliya zimetungwa kwa kutumia mbinu za ki-Aristotle zilizochanganywa na mbinu za jadi za fasihi simulizi. Mbinu za ki-Aristotle ni kama ifuatavyo: msuko, wahusika, maudhui, matumizi ya lugha, muziki na mwonekano ilhali mbinu za jadi za fasihi simulizi ni: utambaji wa hadithi, matambiko, vitendawili, methali, nyimbo, ngonjera na majigambo. Aidha, mtafiti alibaini sababu zalizomfanya Penina Muhando kutumia mbinu za uwili ni kama ifuatavyo: ukombozi wa kisanaa, kutangaza utamaduni wa ki-Afrika na Afrika kwa jumla, na ubunifu. Pia, mtafiti alieleza dhima ya uwili katika tamthiliya teule kama ifutavyo: kuhuisha utamaduni, kuhifadhi historia, mila na desturi, kuhimiza ushirikiano na uhuru wa msanii. Utafiti huu ni changamoto kwa watunzi wa kazi za sanaa katika kuleta mapinduzi ya kimtindo kwa kuingiza mbinu za jadi za ki-Afrika ikiwemo matumizi ya fasihi simulizi iliyokuwa imesahaulika kwa muda mrefu kutokana na athari za wakoloni.Item Mchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu wa Mafia(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Mohamed, Idrissa SaidiUtafiti huu umefanyika katika vijiji vya Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani juu ya mchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu wa Mafia. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha aina za nyimbo za ngoma ya Mdatu na miktadha ambamo zinaimbwa, kubainisha maadili yanayobebwa katika nyimbo za ngoma ya Mdatu na kubainisha namna lugha inavyotumika kuwasilisha ujumbe kwa hadhira kwa kuzingatia maadili ya watu wa Mafia. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali, kama vile, mahojiano, hojaji, majadiliano, uchunguzi makini na mapitio ya maandishi, kisha data hizo zilichambuliwa kwa njia ya maelezo kwa kuzingatia nadharia ya umarksi. Matokeo ya utafiti huu ni mosi, mtafiti amefanikiwa kuzibainisha nyimbo kadhaa za ngoma ya Mdatu, nyimbo ambazo hazikuwahi kubainishwa hapo awali. Vile vile matokeo ya utafiti yameonesha kuwa dhamira katika nyimbo za ngoma ya Mdatu zimeakisi matukio muhimu ya kijamii, kama vile, harusi, jando na unyago na sherehe za kiserikali. Aidha utafiti umebaini kuwa nyimbo za ngoma ya Mdatu zimebeba vipengele mbalimbali vya kimaadili vinavyohimizwa katika jamii ya watu wa Mafia, ambavyo ni suala la uaminifu katika jamii, stara kwa wanawake, malezi bora ya familia, umuhimu wa elimu, kufanya kazi kwa bidii, umuhimu wa kilimo, kujiepusha na fitina na uongo na uaminifu katika ndoa. Mwisho tumebaini kuwa katika ufinyanzi wa nyimbo za ngoma ya Mdatu kuna utajiri mkubwa wa utumizi wa vipengele vya lugha. Kama vile, tamathali za semi, methali, misemo na lahaja ya Mafia. Matokeo ya jumla ya utafiti huu yametoa pendekezo kwa tafiti zaidi zifanyike katika kutafiti na kukusanya nyimbo za ngoma zinazopatikana Mafia.Item Usawiri wa mwanamke katika tamthiliya teule za Penina Muhando(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) George, GraceUtafiti huu umejadili kuhusu Usawiri wa Mwanamke katika Tamthiliya Teule za Penina Mhando. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na hali ya kila siku ya waandishi wa tamthiliya za Kiswahili wakiwemo wanaume, kumkweza mwanaume kinafasi na kimajukumu na kumshusha mwanamke, hivyo utafiti huu ulijikita kuchunguza nafasi ya mwanamke katika tamthilia teule za Penina Muhando. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani kwa kuchunguza kazi mbalimbali ili kupata ruwaza ya jumla kuhusu nafasi ya mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia, pia vitabu teule ambavyo ni Hatia (1972) na Nguzo Mama (1982) vimesomwa na kuchunguzwa kwa makini na kuona jinsi mwanamke alivyochorwa. Mahojiano yalifanyika ili kupata mawazo mbalimbali kuhusu mada ya utafiti. Pia umeongozwa na nadharia ya Ufeministi. Hivyo utafiti huu umebaini kuwa kuna tofauti kubwa za kimajukumu kati ya mwanaume na mwanamke. Kwa upande mmoja mwanamke amechorwa kwa mtazamo hasi na chanya yaani ameonekana ni kiumbe duni, mnyonge, na hivyo kuendelea kumdharau, kumkejeli na kumdhihaki. Kwa upande mwingine mwanamke amechorwa kama mshauri, mlezi, mbunifu, mvumilivu na mtu mwenye huruma na ushirikiano katika jamii. Pia utafiti huu umebaini kuwa zipo athari mbalimbali zinazosababishwa na uchorwaji wa mwanamke katika tamthilia. Athari mojawapo ni kuigwa kwa matendo machafu ambayo yanasababisha kudharaulika na kuendelea kukandamizwa kwa wanawake. Hivyo basi kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa katika jamii nafasi ya mwanamke na mgawawanyo wa majukumu huwa tofauti na mwanaume kwa sababu ya mila na tamaduni mbovu ambazo humchukulia mwanamke kama kiumbe duni wakati wote ingawa uhalisia wa sasa hauko hivyo.Item Tofauti za mtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Mohamed Said Abdulla Na Erick James Shigongo(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Chagaka, Getruda AlexTafiti zilizotangulia zimeonesha kuwajadili wanafasihi hawa wawili, Muhamed Said Abdulla (MSA) na Erick James Shigongo kwa upekee. Mambo kadhaa yamekuwa yakidondolewa katika kazi zao ili kukidhi mahitaji ya tafiti za wakati huo. Kazi nyingi za MSA na Shigongo zimeshughulikiwa ingawa ni kwa viwango mbalimbali. Utafiti huu una jumla ya sura tano ukijaribu kujadili hoja kuwa waandishi wa riwaya ya upelelezi ya Kiswahili wanatofautiana kimtindo. Hivyo, tumejaribu kubainisha tofauti za kimtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili kwa kufanya ulinganisho wa riwaya za Muhamed Said Abdulla (MSA), Mzimu wa Watu wa Kale (1957) na Kosa la Bwana Musa (1984) na riwaya za Erick James Shigongo, Damu na Machozi (2005) na Kifo ni Haki Yangu (2012). Utafiti umebainisha tofauti za kimtindo hususani vipengele vya matumizi ya lugha vilivyojitokeza katika riwaya hizi kwa kuangalia namna walivyotumia vipengele hivi kuumba fani katika kazi zao. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya elimumitindo. Utafiti huu ulijikita zaidi maktabani kwa kudurusu riwaya mbili zilizoteuliwa na mtafiti kwa kila mwandishi, pia kupitia majarida na makala za waandishi mbalimbali walioandika juu ya mtindo na riwaya ya upelelezi. Mbinu iliyotamalaki kutoa matokeo ya utafiti huu ni ya kiufafanuzi katika kuwasilisha mchakato wa data zilizokusanywa maktabani. Njia ya maelezo ndiyo imetumika kutokana na asili ya utafiti wenyewe ulivyo. Hakuna data zilizowasilishwa kwa tarakimu. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa mtindo wa fasihi hutofautiana kati ya mwandishi mmoja na mwingine kutegemeana na jamii, makuzi na mazingira yaliyomzunguka mwandishi. Shabaha mojawapo ya tasnifu hii ni kuhimiza utafutaji katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili.