Dhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: mifano kutoka kwa Wasukuma
Loading...
Date
2014
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Visasili ni hadithi zinazoelezea desturi, itikadi, jadi na dini ambazo watu wa kale
walizifuata (kuzishika) kutokana na mafundisho yaliyotokana na masimulizi hayo,
wakiwa na uwezo wa kufanya miujiza kutokana nguvu za asili. Visasili vina dhima
ya kuelimisha, kuonya, kuburudisha na kuadilisha kama tanzu zingine za fasihi
simulizi.
Utafiti huu ulikusanya visasili na kuchambua amali za kitamaduni za jamii ya
Wasukuma ambazo zinahifadhiwa na kurithishwa katika visasili hivyo. Katika
kukidhi matakwa ya malengo ya utafiti huu, kiunzi cha nadharia ya Masimulizi ya
Mdomo na Uasilia zilitumiwa katika kuchambua data. Data zilikusanywa katika
wilaya ya Magu, Kwimba, Nyamagana na Misungwi. Mbinu ya hojaji ilitumika
sambamba na maandiko mbalimbali kutoka kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha
Dodoma na Dar es Salaam, maandiko yaliyotafiti kuhusu visasili vya jamii
mbalimbali, vilevile, katika kupata wawakilishi utafiti huu ulitumia sampuli lengwa
(ya kimakusudi) kwa kuzingatia sifa za watafitiwa.
Utafiti huu umebaini kuwa, uhifadhi na urithishaji wa fasihi simulizi katika jamii,
utaisaidia kutunza kumbukumbu za asili za jamii ya Wasukuma, kuwasaidia watafiti
katika utanzu huu wa visasili na kupanua mawanda mapana ya uelewa katika jamii.
Visasili kama tanzu zingine za fasihi simulizi, huonesha asili ya jamii husika hasa
kupitia kwenye masimulizi na matambiko. Ni utanzu unaorejesha fikra za
mwanadamu kuona namna wanadamu wa kale walivyoishi kwa kuabudu miungu
waliyoiamini na kuwatatulia matatizo yao. Hakuna jamii ambayo haina historia
yake na utamaduni wake, hivyo, wataalam mbalimbali wa fasihi simulizi wanapaswa
kushughulika katika tafiti mbalimbali ili kupata ukweli wa kila jamii wa desturi na
mila zake.
Description
Tasnifu (MA Kiswahili)
Keywords
Visasili, Hadithi, Desturi, Fasihi simulizi, Amali, Wasukuma, Mwanza, Tanzu fasihi, Fasihi, Jamii wasukuma, Magu, Kwimba, Misungwi, Nyamagana
Citation
Mgunda, J. M. (2014). Dhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: Mifano kutoka kwa Wasukuma (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.