Dhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: mifano kutoka kwa Wasukuma

dc.contributor.authorMgunda, John Madirisha
dc.date.accessioned2020-03-05T07:47:18Z
dc.date.available2020-03-05T07:47:18Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)en_US
dc.description.abstractVisasili ni hadithi zinazoelezea desturi, itikadi, jadi na dini ambazo watu wa kale walizifuata (kuzishika) kutokana na mafundisho yaliyotokana na masimulizi hayo, wakiwa na uwezo wa kufanya miujiza kutokana nguvu za asili. Visasili vina dhima ya kuelimisha, kuonya, kuburudisha na kuadilisha kama tanzu zingine za fasihi simulizi. Utafiti huu ulikusanya visasili na kuchambua amali za kitamaduni za jamii ya Wasukuma ambazo zinahifadhiwa na kurithishwa katika visasili hivyo. Katika kukidhi matakwa ya malengo ya utafiti huu, kiunzi cha nadharia ya Masimulizi ya Mdomo na Uasilia zilitumiwa katika kuchambua data. Data zilikusanywa katika wilaya ya Magu, Kwimba, Nyamagana na Misungwi. Mbinu ya hojaji ilitumika sambamba na maandiko mbalimbali kutoka kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dodoma na Dar es Salaam, maandiko yaliyotafiti kuhusu visasili vya jamii mbalimbali, vilevile, katika kupata wawakilishi utafiti huu ulitumia sampuli lengwa (ya kimakusudi) kwa kuzingatia sifa za watafitiwa. Utafiti huu umebaini kuwa, uhifadhi na urithishaji wa fasihi simulizi katika jamii, utaisaidia kutunza kumbukumbu za asili za jamii ya Wasukuma, kuwasaidia watafiti katika utanzu huu wa visasili na kupanua mawanda mapana ya uelewa katika jamii. Visasili kama tanzu zingine za fasihi simulizi, huonesha asili ya jamii husika hasa kupitia kwenye masimulizi na matambiko. Ni utanzu unaorejesha fikra za mwanadamu kuona namna wanadamu wa kale walivyoishi kwa kuabudu miungu waliyoiamini na kuwatatulia matatizo yao. Hakuna jamii ambayo haina historia yake na utamaduni wake, hivyo, wataalam mbalimbali wa fasihi simulizi wanapaswa kushughulika katika tafiti mbalimbali ili kupata ukweli wa kila jamii wa desturi na mila zake.en_US
dc.identifier.citationMgunda, J. M. (2014). Dhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: Mifano kutoka kwa Wasukuma (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1994
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectVisasilien_US
dc.subjectHadithien_US
dc.subjectDesturien_US
dc.subjectFasihi simulizien_US
dc.subjectAmalien_US
dc.subjectWasukumaen_US
dc.subjectMwanzaen_US
dc.subjectTanzu fasihien_US
dc.subjectFasihien_US
dc.subjectJamii wasukumaen_US
dc.subjectMaguen_US
dc.subjectKwimbaen_US
dc.subjectMisungwien_US
dc.subjectNyamaganaen_US
dc.titleDhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: mifano kutoka kwa Wasukumaen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mgunda, John M.pdf
Size:
909.08 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: