Mchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu wa Mafia
Loading...
Date
2014
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Utafiti huu umefanyika katika vijiji vya Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani juu ya
mchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu
wa Mafia. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha aina za nyimbo za ngoma ya Mdatu
na miktadha ambamo zinaimbwa, kubainisha maadili yanayobebwa katika nyimbo za
ngoma ya Mdatu na kubainisha namna lugha inavyotumika kuwasilisha ujumbe kwa
hadhira kwa kuzingatia maadili ya watu wa Mafia.
Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali, kama vile,
mahojiano, hojaji, majadiliano, uchunguzi makini na mapitio ya maandishi, kisha
data hizo zilichambuliwa kwa njia ya maelezo kwa kuzingatia nadharia ya umarksi.
Matokeo ya utafiti huu ni mosi, mtafiti amefanikiwa kuzibainisha nyimbo kadhaa za
ngoma ya Mdatu, nyimbo ambazo hazikuwahi kubainishwa hapo awali. Vile vile
matokeo ya utafiti yameonesha kuwa dhamira katika nyimbo za ngoma ya Mdatu
zimeakisi matukio muhimu ya kijamii, kama vile, harusi, jando na unyago na sherehe
za kiserikali. Aidha utafiti umebaini kuwa nyimbo za ngoma ya Mdatu zimebeba
vipengele mbalimbali vya kimaadili vinavyohimizwa katika jamii ya watu wa Mafia,
ambavyo ni suala la uaminifu katika jamii, stara kwa wanawake, malezi bora ya
familia, umuhimu wa elimu, kufanya kazi kwa bidii, umuhimu wa kilimo, kujiepusha
na fitina na uongo na uaminifu katika ndoa. Mwisho tumebaini kuwa katika
ufinyanzi wa nyimbo za ngoma ya Mdatu kuna utajiri mkubwa wa utumizi wa
vipengele vya lugha. Kama vile, tamathali za semi, methali, misemo na lahaja ya
Mafia.
Matokeo ya jumla ya utafiti huu yametoa pendekezo kwa tafiti zaidi zifanyike katika
kutafiti na kukusanya nyimbo za ngoma zinazopatikana Mafia.
Description
Tasnifu (MA Kiswahili)
Keywords
Mafia, Maadili, Nyimbo, Ngoma, Dhamira, Harusi, Unyago, Jando, Ngoma mdatu, Jamii wamafia
Citation
Mohamed, I. S. (2014). Mchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu wa Mafia (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.