Mchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu wa Mafia

dc.contributor.authorMohamed, Idrissa Saidi
dc.date.accessioned2020-03-05T07:37:42Z
dc.date.available2020-03-05T07:37:42Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umefanyika katika vijiji vya Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani juu ya mchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu wa Mafia. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha aina za nyimbo za ngoma ya Mdatu na miktadha ambamo zinaimbwa, kubainisha maadili yanayobebwa katika nyimbo za ngoma ya Mdatu na kubainisha namna lugha inavyotumika kuwasilisha ujumbe kwa hadhira kwa kuzingatia maadili ya watu wa Mafia. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali, kama vile, mahojiano, hojaji, majadiliano, uchunguzi makini na mapitio ya maandishi, kisha data hizo zilichambuliwa kwa njia ya maelezo kwa kuzingatia nadharia ya umarksi. Matokeo ya utafiti huu ni mosi, mtafiti amefanikiwa kuzibainisha nyimbo kadhaa za ngoma ya Mdatu, nyimbo ambazo hazikuwahi kubainishwa hapo awali. Vile vile matokeo ya utafiti yameonesha kuwa dhamira katika nyimbo za ngoma ya Mdatu zimeakisi matukio muhimu ya kijamii, kama vile, harusi, jando na unyago na sherehe za kiserikali. Aidha utafiti umebaini kuwa nyimbo za ngoma ya Mdatu zimebeba vipengele mbalimbali vya kimaadili vinavyohimizwa katika jamii ya watu wa Mafia, ambavyo ni suala la uaminifu katika jamii, stara kwa wanawake, malezi bora ya familia, umuhimu wa elimu, kufanya kazi kwa bidii, umuhimu wa kilimo, kujiepusha na fitina na uongo na uaminifu katika ndoa. Mwisho tumebaini kuwa katika ufinyanzi wa nyimbo za ngoma ya Mdatu kuna utajiri mkubwa wa utumizi wa vipengele vya lugha. Kama vile, tamathali za semi, methali, misemo na lahaja ya Mafia. Matokeo ya jumla ya utafiti huu yametoa pendekezo kwa tafiti zaidi zifanyike katika kutafiti na kukusanya nyimbo za ngoma zinazopatikana Mafia.en_US
dc.identifier.citationMohamed, I. S. (2014). Mchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu wa Mafia (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1991
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectMafiaen_US
dc.subjectMaadilien_US
dc.subjectNyimboen_US
dc.subjectNgomaen_US
dc.subjectDhamiraen_US
dc.subjectHarusien_US
dc.subjectUnyagoen_US
dc.subjectJandoen_US
dc.subjectNgoma mdatuen_US
dc.subjectJamii wamafiaen_US
dc.titleMchango wa nyimbo za ngoma ya Mdatu katika kudumisha maadili ya jamii ya watu wa Mafiaen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Idrissa Saidi Mohamed.pdf
Size:
714.25 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: