Tofauti za mtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Mohamed Said Abdulla Na Erick James Shigongo
Loading...
Date
2014
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Tafiti zilizotangulia zimeonesha kuwajadili wanafasihi hawa wawili, Muhamed Said
Abdulla (MSA) na Erick James Shigongo kwa upekee. Mambo kadhaa yamekuwa
yakidondolewa katika kazi zao ili kukidhi mahitaji ya tafiti za wakati huo. Kazi
nyingi za MSA na Shigongo zimeshughulikiwa ingawa ni kwa viwango mbalimbali.
Utafiti huu una jumla ya sura tano ukijaribu kujadili hoja kuwa waandishi wa riwaya
ya upelelezi ya Kiswahili wanatofautiana kimtindo. Hivyo, tumejaribu kubainisha
tofauti za kimtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili kwa kufanya ulinganisho
wa riwaya za Muhamed Said Abdulla (MSA), Mzimu wa Watu wa Kale (1957) na
Kosa la Bwana Musa (1984) na riwaya za Erick James Shigongo, Damu na Machozi
(2005) na Kifo ni Haki Yangu (2012). Utafiti umebainisha tofauti za kimtindo
hususani vipengele vya matumizi ya lugha vilivyojitokeza katika riwaya hizi kwa
kuangalia namna walivyotumia vipengele hivi kuumba fani katika kazi zao. Utafiti
huu umeongozwa na nadharia ya elimumitindo.
Utafiti huu ulijikita zaidi maktabani kwa kudurusu riwaya mbili zilizoteuliwa na
mtafiti kwa kila mwandishi, pia kupitia majarida na makala za waandishi mbalimbali
walioandika juu ya mtindo na riwaya ya upelelezi. Mbinu iliyotamalaki kutoa
matokeo ya utafiti huu ni ya kiufafanuzi katika kuwasilisha mchakato wa data
zilizokusanywa maktabani. Njia ya maelezo ndiyo imetumika kutokana na asili ya
utafiti wenyewe ulivyo. Hakuna data zilizowasilishwa kwa tarakimu. Matokeo ya
utafiti yamebainisha kuwa mtindo wa fasihi hutofautiana kati ya mwandishi mmoja
na mwingine kutegemeana na jamii, makuzi na mazingira yaliyomzunguka
mwandishi. Shabaha mojawapo ya tasnifu hii ni kuhimiza utafutaji katika maendeleo
ya fasihi ya Kiswahili.
Description
Tasnifu (MA Kiswahili)
Keywords
Muhamed Said Abdulla, Riwaya, Upelelezi, Kiswahili, Fasihi andishi, Lugha, Riwaya kiswahili, Riwaya upelelezi, Eric James Shigongo, Ulinganisho riwaya, Maendeleo fasihi, Maendeleo kiswahili, Fani, Maudhui
Citation
Chagaka, G. A. (2014). Tofauti za mtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Mohamed Said Abdulla Na Erick James Shigongo (Tasnifu) Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.