Tofauti za mtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Mohamed Said Abdulla Na Erick James Shigongo

dc.contributor.authorChagaka, Getruda Alex
dc.date.accessioned2020-03-05T07:35:46Z
dc.date.available2020-03-05T07:35:46Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTafiti zilizotangulia zimeonesha kuwajadili wanafasihi hawa wawili, Muhamed Said Abdulla (MSA) na Erick James Shigongo kwa upekee. Mambo kadhaa yamekuwa yakidondolewa katika kazi zao ili kukidhi mahitaji ya tafiti za wakati huo. Kazi nyingi za MSA na Shigongo zimeshughulikiwa ingawa ni kwa viwango mbalimbali. Utafiti huu una jumla ya sura tano ukijaribu kujadili hoja kuwa waandishi wa riwaya ya upelelezi ya Kiswahili wanatofautiana kimtindo. Hivyo, tumejaribu kubainisha tofauti za kimtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili kwa kufanya ulinganisho wa riwaya za Muhamed Said Abdulla (MSA), Mzimu wa Watu wa Kale (1957) na Kosa la Bwana Musa (1984) na riwaya za Erick James Shigongo, Damu na Machozi (2005) na Kifo ni Haki Yangu (2012). Utafiti umebainisha tofauti za kimtindo hususani vipengele vya matumizi ya lugha vilivyojitokeza katika riwaya hizi kwa kuangalia namna walivyotumia vipengele hivi kuumba fani katika kazi zao. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya elimumitindo. Utafiti huu ulijikita zaidi maktabani kwa kudurusu riwaya mbili zilizoteuliwa na mtafiti kwa kila mwandishi, pia kupitia majarida na makala za waandishi mbalimbali walioandika juu ya mtindo na riwaya ya upelelezi. Mbinu iliyotamalaki kutoa matokeo ya utafiti huu ni ya kiufafanuzi katika kuwasilisha mchakato wa data zilizokusanywa maktabani. Njia ya maelezo ndiyo imetumika kutokana na asili ya utafiti wenyewe ulivyo. Hakuna data zilizowasilishwa kwa tarakimu. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa mtindo wa fasihi hutofautiana kati ya mwandishi mmoja na mwingine kutegemeana na jamii, makuzi na mazingira yaliyomzunguka mwandishi. Shabaha mojawapo ya tasnifu hii ni kuhimiza utafutaji katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili.en_US
dc.identifier.citationChagaka, G. A. (2014). Tofauti za mtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Mohamed Said Abdulla Na Erick James Shigongo (Tasnifu) Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1988
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectMuhamed Said Abdullaen_US
dc.subjectRiwayaen_US
dc.subjectUpelelezien_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectFasihi andishien_US
dc.subjectLughaen_US
dc.subjectRiwaya kiswahilien_US
dc.subjectRiwaya upelelezien_US
dc.subjectEric James Shigongoen_US
dc.subjectUlinganisho riwayaen_US
dc.subjectMaendeleo fasihien_US
dc.subjectMaendeleo kiswahilien_US
dc.subjectFanien_US
dc.subjectMaudhuien_US
dc.titleTofauti za mtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Mohamed Said Abdulla Na Erick James Shigongoen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
GETRUDA ALEX CHAGAKA.pdf
Size:
667.16 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: