Usawiri wa jinsi ya kiume katika riwaya teule za Shafi Adam Shafi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2020
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Tasinifu hii inahusiana na usawiri wa jinsi ya kiume katika riwaya teule za Shafi Adam Shafi. Tasinifu hii imejengwa na malengo matatu yafuatayo: kubainisha namna jinsi ya kiume ilivyosawiriwa katika riwaya za Shafi Adam Shafi. Pia, kubainisha changamoto zinazoikabili jinsi ya kiume katika riwaya za Shafi Adam Shafi. Lengo la tatu, ni kuelezea mbinu zilizotumiwa na jinsi ya kiume katika kukabiliana na changamoto hizo. Matokeo ya utafiti uliofanyika yametolewa kwa kuzingatia malengo na maswali ya utafiti kwa kuongozwa na nadharia ya uhalisia. Kuhusu lengo la kwanza, utafiti umebaini kuwa, jinsi ya kiume inasawiriwa kama jinsi yenye ujasiri, uvumilivu, msimamo, uongozi, wanamapinduzi na katili. Kuhusu lengo la pili, utafiti umebaini kuwa, umebainisha changamoto kama: kukosa elimu, hali ngumu ya maisha, usaliti, kukosa haki na kutenganishwa na familia. Kuhusu lengo la tatu, utafiti umebaini kuwa, mbinu kama: kutafuta burudani, kushirikiana, kudai haki zao (migomo) na kutoroka shida; ni baadhi ya mbinu zinazotumiwa na jinsi ya kiume kukabiliana na changamoto husika. Kukamilika kwa tasinifu hii kumetoa mchango mpya katika uwanja wa fasihi ya Kiswahili. Kwanza, kuipa jinsi ya kiume nafasi ya kutazamwa kama ambavyo jinsi ya kike inatazamwa. Pia, kubainisha changamoto zinazoikabili jinsi ya kiume katika kuhakikisha wanafikia malengo yao. Tatu, tasinifu hii imetoa mwanga katika masuala yanayohusiana na masuala ya jinsi katika fasihi ya Kiswahili.
Description
Tasnifu (Shahada ya Umahiri katika Kiswahili)
Keywords
Jinsi, Jinsia, Kiswahili, Jinsi ya kiume, Shafi Adam Shafi riwaya, Riwaya, Riwaya teule, Fasihi ya kiswahili
Citation
Bayyo, F. B. (2020). Usawiri wa jinsi ya kiume katika riwaya teule za Shafi Adam Shafi (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.