Browsing by Author "Chagaka, Getruda Alex"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Tofauti za mtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Mohamed Said Abdulla Na Erick James Shigongo(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Chagaka, Getruda AlexTafiti zilizotangulia zimeonesha kuwajadili wanafasihi hawa wawili, Muhamed Said Abdulla (MSA) na Erick James Shigongo kwa upekee. Mambo kadhaa yamekuwa yakidondolewa katika kazi zao ili kukidhi mahitaji ya tafiti za wakati huo. Kazi nyingi za MSA na Shigongo zimeshughulikiwa ingawa ni kwa viwango mbalimbali. Utafiti huu una jumla ya sura tano ukijaribu kujadili hoja kuwa waandishi wa riwaya ya upelelezi ya Kiswahili wanatofautiana kimtindo. Hivyo, tumejaribu kubainisha tofauti za kimtindo katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili kwa kufanya ulinganisho wa riwaya za Muhamed Said Abdulla (MSA), Mzimu wa Watu wa Kale (1957) na Kosa la Bwana Musa (1984) na riwaya za Erick James Shigongo, Damu na Machozi (2005) na Kifo ni Haki Yangu (2012). Utafiti umebainisha tofauti za kimtindo hususani vipengele vya matumizi ya lugha vilivyojitokeza katika riwaya hizi kwa kuangalia namna walivyotumia vipengele hivi kuumba fani katika kazi zao. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya elimumitindo. Utafiti huu ulijikita zaidi maktabani kwa kudurusu riwaya mbili zilizoteuliwa na mtafiti kwa kila mwandishi, pia kupitia majarida na makala za waandishi mbalimbali walioandika juu ya mtindo na riwaya ya upelelezi. Mbinu iliyotamalaki kutoa matokeo ya utafiti huu ni ya kiufafanuzi katika kuwasilisha mchakato wa data zilizokusanywa maktabani. Njia ya maelezo ndiyo imetumika kutokana na asili ya utafiti wenyewe ulivyo. Hakuna data zilizowasilishwa kwa tarakimu. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa mtindo wa fasihi hutofautiana kati ya mwandishi mmoja na mwingine kutegemeana na jamii, makuzi na mazingira yaliyomzunguka mwandishi. Shabaha mojawapo ya tasnifu hii ni kuhimiza utafutaji katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili.