Humanities
Permanent URI for this community
Browse
Browsing Humanities by Subject "Ally Choki"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Ujumi katika muziki wa dansi: mfano kutoka nyimbo teule za Marijani Rajabu na Ally Choki(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2015) Laswai, AgripinaTasnifu hii ni matokeo ya utafiti uliojigeza katika kuchambua vipengele vya kiujumi katika muziki wa dansi wa wanamuziki wawili Marijani Rajabu na Ally Choki. Utafiti ulilenga kuchunguza ujumi katika muziki wa dansi wa Tanzania ili kuthibitisha kuwa taaluma ya ujumi ina nafasi kubwa katika kazi za muziki wa dansi. Pia tasnifu hii imejaribu kuona ni kwa kiasi gani, kazi hizo zenye mwelekeo wa kiujumi zinafungamana na idili za jamii ya Watanzania. Aidha imejaribu kutathimini dhima ya vipengele vya kiujumi katika fani na maudhui ya nyimbo za wanamuziki teule. Njia zilizotumika kukusanya data ni kutalii uwandani na udurusi wa kimaktaba. Uchambuzi wa data ulifanywa kwa njia ya ufafanuzi. Data zilizopatikana ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo, halikadhalika, vielelezo vilitumika kwa kiasi kidogo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Kimarx. Nadharia ya Kimarx imetoa mwongozo wa kuchunguza utamaduni na maisha ya watu weusi kwa ujumla. Matokeo ya utafiti huu yameleta mchango mpya wa kitaaluma katika Fasihi ya Kiswahili. Tasnifu imebainisha kuwa uzuri hutambuliwa kwa namna tofauti kati ya jamii moja na nyingine, na ili kuyachambua vyema masuala ya kiujumi, hutupasa kujua idili za jamii husika.Tumebainisha muktadha wa utunzi wa muziki wa dansi kwa jamii ya wakati huu wa maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia. Miongoni mwa michango ni pamoja na matumizi ya idili, adabu na utiifu na umoja katika kufafanua uzuri wa kiujumi katika muziki wa dansi. Aidha, tumetathimini dhima ya vipengele vya kiujumi katika fani na maudhui ya nyimbo teule za Marijani Rajani na Ally Choki. Dhima hizo ni kuelimisha, kuburudisha, kutambulisha jamii na kuonyesha nafasi ya mwanamke katika jamii.