Master Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Master Dissertations by Subject "Andanenga"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mchango wa Andanenga katika ushairi wa Kiswahili(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2015) Kanema, Salum AbdallahTasnifu hii, imejikita katika kuangalia na kuchunguza mchango wa Andanenga katika ushairi wa Kiswahili. Tasnifu hii imejielekeza zaidi katika kuangalia na kuchunguza mchango wa kidhamira na kimuundo katika ushairi wa mwandishi huyu. Kuna mchango mkubwa wa ushairi wa Andanenga katika ushairi wa Kiswahili, lakini tafiti na tahakiki za kina hazijafanyika bado juu ya mshairi huyu mwenye ulemavu wa macho. Ingawa tafiti na tahakiki nyingi zimefanywa kuhusu ushairi wa Kiswahili na maisha ya washairi, bado tafiti na tahakiki nyingi hazijamuangalia kwa jicho yakinifu mshairi huyu. Kutokana na hilo, mtafiti wa kazi hii aliona kuna haja ya kufanya utafiti kwa kina zaidi ili kubaini mchango wa mwandishi huyu katika kuendeleza ushairi wa Kiswahili hasa katika kubaini mchango wake wa kidhamira na kimuundo katika ushairi wa Kiswahili. Lakini pia kuna haja ya kujua mbari yake na maisha ya mshairi huyu. Asilimia kubwa ya utafiti huu ulifanyika maktabani na udurusi wa vitabu teule vya mwandishi huyu ambavyo ni Diwani ya Ustadh (1993) na Bahari ya Elimu ya Ushairi (2002). Kadhalika mtafiti pia alikwenda uwandani kukutana na baadhi ya watu wa karibu wa mtafitiwa na kuhojiana na mtafitiwa mwenyewe. Pia, baadhi ya maeneo ikiwemo TATAKI ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilitembelewa ili kupata taarifa zaidi. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa Andanenga ana mchango mkubwa katika ushairi wa Kiswahili kidhamira na kimuundo. Kidhamira, yanaonekena mambo mengi yaliyojadiliwa na mshairi huyu katika mashairi yake yanasadifu na kuhalisika katika maisha ya kila siku ya jamii ya Watanzania. Kimuundo, ameweza kubainisha miundo changamani ya ushairi wa Kiswahili na kupata mitindo anuai katika ushairi huu. Ameonesha ustadi wake katika usanaji wa miundo na mitindo ya ushairi wa Kiswahili, ya zamani, ya sasa na mipya hivyo kuupa hadhi ushairi huu.