Nyimbo za harusi na maadili ya ndoa za Wapemba

Loading...
Thumbnail Image
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Utafiti huu umechunguza namna dhima za nyimbo za harusi zinavyojenga maadili ya maisha ya ndoa ya jamii ya Kipemba. Aidha umejikita kuchunguza nyimbo za asili za harusi za Kipemba kwa kuzingatia tukio na muhusika na umebainisha dhamira zinazopatikana katika nyimbo hizo ili kuonesha dhima za nyimbo za harusi katika kujenga maadili ya jamii ya Wapemba. Kazi hii imetafitiwa kisiwani Pemba katika mikoa yote miwili, Kaskazini na Kusini. Kutoka mkoa wa kusini data zilikusanywa Tibirinzi na Pujini. Aidha kutoka mkoa wa Kaskazini utafiti ulifanyika maeneo ya Finya, Mlindo na Piki kwa kupata data sahihi kwa muda muafaka. Upatikanaji wa data ulikuwa kwa njia ya usaili na ushiriki na uchunguzi makini. Njia hizi zilitumika ili kupata data zilizo sahihi kwa urahisi. Uchambuzi wa data hizo umefanyika kwa kutumia mbinu ya maelezo iliyoambatana na mbinu ya ufafanuzi. Utafiti huu umegundua kwamba kuna aina tano za nyimbo za harusi katika jamii ya Wapemba. Dhamira na dhima za nyimbo hizo zinaonekana kujenga maadili ya wanandoa wa Kipemba pindi zikiimbwa kwa mnasaba wa kufunza wanandoa lakini kwa sasa zimeshindwa kutimiza wajibu huo kutokana na kutoimbwa kwa mnasaba huo.
Description
Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
Keywords
Nyimbo, Nyimbo za harusi, Maadili, Ndoa, Ndoa za wapemba, Wapemba
Citation
Juma, F. N.(2015). Nyimbo za harusi na maadili ya ndoa za Wapemba. Dodoma: Chuo kikuu cha Dodoma