Uibukaji wa U-nigeria katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania: masuala muhimu ya kuzingatia

dc.contributor.authorKasiga, Gerevaz. A.
dc.date.accessioned2023-10-12T13:42:19Z
dc.date.available2023-10-12T13:42:19Z
dc.date.issued2023
dc.descriptionAbstract. Full text article available at. https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.93en_US
dc.description.abstractImebainika kuwa tasnia ya muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania imetekwa na utamaduni wa nje hususani wa Kinigeria (Mrikaria, 2007; Kasiga, 2022). Athari zake zimebainika katika vipengele kadhaa vya kibunifu (Kasiga, 2021). Pia, misukumo mbalimbali inayowasukuma wasanii kutumia U-Nigeria imebainishwa (Kasiga, 2022). Kimsingi, hali hii inatishia utambulisho wa Kitanzania katika sanaa. Hivyo, makala hii imetoa mapendekezo ya kiuboreshaji dhidi ya UNigeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania. Mapendekezo yaliyotolewa yamehusisha: kufanyika uwekezaji wa muziki wa asili wa Kitanzania, kufanyika kwa usimamizi maalumu katika vyombo vya habari, kuwepo kwa sheria na kanuni za kulinda uasili wa muziki wa kizazi kipya, na uanzishwaji wa semina, warsha pamoja na madarasa maalumu kwa wasanii. Isitoshe, makala imependekeza kuwepo kwa agenda mahususi ya kitaifa kujenga uzalendo, kumakinikia mitindo ya sanaa za Kitanzania katika utengenezaji wa muziki, kuharakisha upatikanaji wa vazi la taifa, kuanzishwa kwa vipindi vya uchambuzi wa nyimbo, na wasanii kushawishiwa kutumia mandhari ya Kitanzania katika video zao. Zaidi, imependekezwa kuanzishwa kwa matamasha na tuzo za muziki, asasi za elimu kutengeneza mitaala ya biashara, lugha ya Kiswahili, na utamaduni wa Kitanzania, na kuwe na muumano kati ya biashara, utamaduni na teknolojia.en_US
dc.identifier.citationKasiga, G. A. (2023). Uibukaji wa U-Nigeria katika Tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania: Masuala Muhimu ya Kuzingatia. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 1(1), 18-30.en_US
dc.identifier.otherDOI: https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.93
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/4171
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherUtafiti Foundationen_US
dc.subjectUibukajien_US
dc.subjectU-Nigeriaen_US
dc.subjectTasniaen_US
dc.subjectTasnia ya Muzikien_US
dc.subjectKizazi Kipyaen_US
dc.subjectMuziki wa Kizazi Kipyaen_US
dc.subjectmuziki wa kizazi kipya wa Kiswahilien_US
dc.subjectmuziki wa asilien_US
dc.subjectsanaa za Kitanzaniaen_US
dc.subjectutengenezaji wa muzikien_US
dc.titleUibukaji wa U-nigeria katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania: masuala muhimu ya kuzingatiaen_US
dc.typeArticleen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Kasiga, G. A. (2023). Uibukaji wa U-Nigeria katika Tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Masuala Muhimu ya Kuzingatia. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 1(1), 18-30..pdf
Size:
90.76 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections