Ontolojia ya kiafrika katika mbolezi za wanyasa

dc.contributor.authorKaponda, George John
dc.date.accessioned2019-08-19T07:54:46Z
dc.date.available2019-08-19T07:54:46Z
dc.date.issued2018
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu Ontolojia ya Kiafrika katika Mbolezi za Wanyasa. Utafiti huu ulifanywa uwandani na maktabani ambapo uwandani, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, ushuhudiaji na mjadala wa vikundi. Kwa upande wa maktabani mtafiti alitumia mbinu ya udurusu maktaba.Utafiti uliongozwa na lengo kuu ambalo ni kubaini vipengele vya ontolojia ya Kiafrika katika mbolezi za Wanyasa. Malengo mahususi ambayo ni; kubainisha aina ya mbolezi zinazopatikana katika jamii ya Wanyasa, kubainisha vipengele vya ontolojia ya Kiafrika ya katika mbolezi za Wanyasa na kutathimini umuhimu wa ontolojia ya Kiafrika kwa jamii ya Wanyasa na Waafrika kwa ujumla. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Ontolojia, mtafiti alikusanya mbolezi na dhana mbalimbali za ontolojia ya Kiafrika katika jamii ya Wanyasa. Jumla ya watafitiwa walioshiriki ni mia moja. Katika data zilizokusanywa, vipengele vilivyojitokeza vilijenga msingi wa data kuu iliyofanyiwa uchambuzi na kujadiliwa. Matokeo yanaonesha kuwa mbolezi zimegawanyika kulingana na vigezo vya chimbuko, rika na wakati. Katika chimbuko kuna mbolezi za asili na mbolezi changamani. Katika rika kuna mbolezi za watoto na mbolezi za watu wazima. Aidha, katika wakati kuna mbolezi za mara baada ya msiba kutokea, buriani, ibada ya mazishi na mazishi. Vipengele vya ontolojia ya Kiafrika vilivyobainishwa ni Mungu, ardhi, roho, kifo, mizimu na utu. Vipengele hivi vimebainika kuwa vimejengwa kiherakia na kutegemeana katika nguvu ijulikanayo kama kani uhai. Aidha, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa jamii inaendelea kudumisha umoja na mshikamano, kurithisha amali, kulinda maadili, kutolea elimu na utambulisho wa jamii. Utafiti huu umependekeza tafiti nyingi zaidi ziendelee kufanyika kuhusiana na ontolojia ya Kiafrika katika fasihi simulizi.en_US
dc.identifier.citationKaponda, G. J. (2018). Ontolojia ya kiafrika katika mbolezi za wanyasa (Tasnifu shahada ya Kiswahili). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/858
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectOntolojiaen_US
dc.subjectMbolezien_US
dc.subjectUdurusuen_US
dc.subjectRikaen_US
dc.subjectMunguen_US
dc.subjectRohoen_US
dc.subjectKifoen_US
dc.subjectMizimuen_US
dc.subjectUtuen_US
dc.subjectAfricaen_US
dc.subjectUmojaen_US
dc.subjectMshikamano,en_US
dc.subjectAmalien_US
dc.subjectMaadili,en_US
dc.subjectFasihi simulizien_US
dc.subjectWanyasaen_US
dc.subjectAsilien_US
dc.subjectChangamanien_US
dc.subjectKiherakiaen_US
dc.subjectKani uhaien_US
dc.subjectNadhariaen_US
dc.subjectMsibaen_US
dc.titleOntolojia ya kiafrika katika mbolezi za wanyasaen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Kaponda, George John.pdf
Size:
2.38 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: