Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka vitendawili vya Kiswahili

dc.contributor.authorNgatungwa, Felista J.
dc.date.accessioned2021-05-04T11:55:22Z
dc.date.available2021-05-04T11:55:22Z
dc.date.issued2020
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii inayoitwa “Usawiri wa Falsafa ya Kiafrika katika Semi: Mifano kutoka Vitendawili vya Kiswahili” iliongozwa na malengo mahsusi matatu. Nayo ni, mosi, kubainisha vijenzi vya falsafa ya Kiafrika katika muktadha wa kitamaduni. Pili, kujadili falsafa ya Kiafrika kama inavyojitokeza katika vitendawili vya Kiswahili na tatu, kutathmini athari ya falsafa ya Kiafrika kwa jamii kama inavyosawiriwa katika vitendawili vya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Kisosholojia kupitia misingi yake kama ilivyofafanuliwa katika utafiti huu. Nadharia hii ilitumika katika michakato ya ukusanyaji wa data, uchambuzi na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti. Utafiti huu ni wa kitaamuli, umetumia usanifu wa kifenomenolojia katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Utafiti huu ulifanywa uwandani na maktabani. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, mijadala ya vikundi lengwa na udurusu wa nyaraka. Eneo la utafiti lilihusisha mikoa ya Kagera na Dodoma. Sampuli ya utafiti iligawiwa katika makundi matatu. Nayo ni wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, wanajamii wenye umri kuanzia miaka hamsini na tano na kuendelea na maandiko kuhusu vitendawili vya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika. Sampuli ilipatikana kwa kutumia mbinu ya sampuli lengwa ya mpokezo na wa kutegemeafursa. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa falsafa ya Kiafrika hudhihirika kupitia mambo mbalimbali yanayojitokeza katika maisha ya mwanadamu. Mambo hayo ni suala la umoja na ushirikiano, ndoa na uzazi, “uchawi na ushirikina”, uhai na kifo, uduara, maadili na suala la imani katika Mungu na mizimu. Aidha, kupitia mifano mbalimbali ya vitendawili vya Kiswahili, utafiti umebaini kuwa, utanzu wa vitendawili una hazina kubwa katika kuhifadhi na kutunza maarifa ya falsafa ya Kiafrika na pia falsafa hiyo ina athari kubwa katika maisha ya jamii ya Kiafrika. Utafiti umependekeza kuwa bado kuna haja ya tafiti nyingi zaidi kufanyika katika uga wa fasihi simulizi, ili kubaini ni kwa namna gani tanzu za fasihi hiyo zinaweza kutumika kama darasa la kufunza na kuhifadhi maarifa ya kifalsafa ya jamii za Waafrika.en_US
dc.identifier.citationNgatungwa, F. J. (2020). Usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka vitendawili vya Kiswahili (Tasnifu ya Umahiri). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/2919
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherThe University of Dodomaen_US
dc.subjectSemien_US
dc.subjectVitendawilien_US
dc.subjectFalsafaen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectKiafrikaen_US
dc.subjectKiafrika falsafaen_US
dc.subjectVitendawili kiswahilien_US
dc.subjectVijenzi falsafaen_US
dc.titleUsawiri wa falsafa ya Kiafrika katika semi: mifano kutoka vitendawili vya Kiswahilien_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
FELISTAJ.NGATUNGWA.pdf
Size:
3.37 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: