Matumizi na dhima ya uwili katika tamthiliya za kiswahili: Mifano kutoka katika tamthiliya teule za Penina Muhando (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.

dc.contributor.authorStephen, Jeremiah
dc.date.accessioned2020-03-05T07:42:05Z
dc.date.available2020-03-05T07:42:05Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu Uwili katika Tamthiliya za Kiswahili kwa kuangalia Tamthiliya teule za Penina Muhando. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kuchambua tamthiliya teule za Penina Muhando ili kubainisha matumizi ya uwili katika tamthiliya hizo, kueleza sababu zilizomfanya Penina Muhando kutumia mbinu za uwili katika utunzi wa tamthiliya teule, kadhalika kueleza dhima ya uwili katika tamthiliya teule za Penina Muhando. Katika utafiti huu, data zilikusanywa uwandani na maktabani. Baada ya hapo mtafiti alitumia mkabala wa maelezo katika kuchanganua data huku akiongozwa na nadharia ya Ujumi Mweusi. Utafiti huu ulibaini kuwa katika tamthiliya teule za Penina Muhando kuna uwili, yaani tamthiliya zimetungwa kwa kutumia mbinu za ki-Aristotle zilizochanganywa na mbinu za jadi za fasihi simulizi. Mbinu za ki-Aristotle ni kama ifuatavyo: msuko, wahusika, maudhui, matumizi ya lugha, muziki na mwonekano ilhali mbinu za jadi za fasihi simulizi ni: utambaji wa hadithi, matambiko, vitendawili, methali, nyimbo, ngonjera na majigambo. Aidha, mtafiti alibaini sababu zalizomfanya Penina Muhando kutumia mbinu za uwili ni kama ifuatavyo: ukombozi wa kisanaa, kutangaza utamaduni wa ki-Afrika na Afrika kwa jumla, na ubunifu. Pia, mtafiti alieleza dhima ya uwili katika tamthiliya teule kama ifutavyo: kuhuisha utamaduni, kuhifadhi historia, mila na desturi, kuhimiza ushirikiano na uhuru wa msanii. Utafiti huu ni changamoto kwa watunzi wa kazi za sanaa katika kuleta mapinduzi ya kimtindo kwa kuingiza mbinu za jadi za ki-Afrika ikiwemo matumizi ya fasihi simulizi iliyokuwa imesahaulika kwa muda mrefu kutokana na athari za wakoloni.en_US
dc.identifier.citationStephen, J. (2014). Matumizi na dhima ya uwili katika tamthiliya za kiswahili: mifano kutoka katika tamthiliya teule za Penina Muhando (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1992
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectUjumien_US
dc.subjectAristotleen_US
dc.subjectFasihi andishien_US
dc.subjectFasihi simulizien_US
dc.subjectMatambikoen_US
dc.subjectUtamadunien_US
dc.subjectMatambikoen_US
dc.subjectTamthiliyaen_US
dc.subjectPenina Muhandoen_US
dc.subjectMatumizi uwilien_US
dc.subjectNadharia ujumi mweusien_US
dc.subjectTanzu fasihien_US
dc.subjectHistoria fasihien_US
dc.subjectUtamaduni Afrikaen_US
dc.titleMatumizi na dhima ya uwili katika tamthiliya za kiswahili: Mifano kutoka katika tamthiliya teule za Penina Muhando (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Jeremiah Stephen.pdf
Size:
766.35 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: