Ubantuishaji wa kimofolojia katika vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu

dc.contributor.authorHakimu, Johari
dc.date.accessioned2021-03-02T07:38:08Z
dc.date.available2021-03-02T07:38:08Z
dc.date.issued2020
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Zamivu katika Kiswahili)en_US
dc.description.abstractPamoja na kwamba lugha ya Kiswahili ina maneno mengi yaliyokopwa katika lugha ya Kiarabu, haijawa wazi ni kwa namna gani maneno hayo (hasa vitenzi) ya Kiswahili yenye asili ya Kiarabu yamepata sifa za Kibantu. Kwa hiyo, kuna masuala kadhaa kuhusu ubantuishaji wa vitenzi vya mkopo ambayo hayajawa wazi. Masuala hayo ni kama vile ubainishaji wa maumbo ya vitenzi, ufafanuzi wa michakato ya kimofolojia inayopitiwa katika ubantuishaji wa vitenzi hivyo, na tathmini ya mwelekeo wa ubantuishaji wa vitenzi hivyo. Utafiti ulifanyika katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo ulihusisha maeneo ya Tanzania bara na Zanzibar. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa njia tatu ambazo ni: upitiaji wa nyaraka, usaili na upimaji wa usahihi wa kisarufi. Katika uchanganuzi na ufasiri wa data, Nadharia ya Mofolojia Leksika na Nadharia ya Usarufishaji zilitumika. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, msambao wa vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu katika ruwaza ya vitenzi vya Kibantu unachukua maumbo kumi (10) kati ya kumi na moja (11) ya ruwaza hiyo sawa na vitenzi vya Kiswahili asilia. Tofauti kubwa ya vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu imebainika katika baadhi ya michakato ya ubantuishaji ya vitenzi hivyo. Vilevile, viambishi vya vitenzi vimechanganuliwa katika darajia nne zenye kuakisi michakato ya unyambuzi au uambatizi wa viambishi husika. Darajia hizi pia zinaakisi viwango vya ukale wa viambishi vya Kiswahili. Ukale huo umepimwa kwa enzi za kabla ya Kiswahili kukutana na Kiarabu. Baadhi ya viambishi visivyojitokeza katika vitenzi vyenye asili ya Kiarabu ni vyenye ukale wa zamani zaidi, na kwamba michakato yake kimofolojia na kifonolojia ilishakoma kabla Kiarabu kukutana na Kiswahili. Pia, vitenzi vilivyochanganuliwa kimofolojia, mwelekeo wake wa ubantuishaji umebainika kwa kutumia Nadharia ya Usarufishaji. Kutokana na nadharia hiyo, ukamilifu na usiukamilifu wa ubantuinshaji wa vitenzi hivyo umebainishwa. Ukamilifu na usiukamilifu umebainika kutokana na matumizi ya ruwaza ya vitenzi vya Kibantu na michakato ya ubantuishaji. Kwa kuwa utafiti huu umechunguza vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu, tafiti zijazo zinaweza kuchunguza aina nyingine za maneno. Hata hivyo, kwa kuwa usarufishaji hufanyika taratibu halikutolewa hitimisho la kuonesha ubantuishaji wa vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu unapokomea.en_US
dc.identifier.citationHakimu, J. (2020). Ubantuishaji wa kimofolojia katika vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabu (Tasnifu ya uzamivu ). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/2855
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectMofolojiaen_US
dc.subjectVitenzien_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectKiarabuen_US
dc.subjectKibantuen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.subjectLughaen_US
dc.subjectUbantuishajien_US
dc.titleUbantuishaji wa kimofolojia katika vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya Kiarabuen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
JOHARI HAKIMU.pdf
Size:
2.95 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: