Matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahli: Ulinganisho wa Kichomi na Tungizi za Mnyagatwa

dc.contributor.authorKalinga, Joyce
dc.date.accessioned2021-03-02T07:34:16Z
dc.date.available2021-03-02T07:34:16Z
dc.date.issued2020
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Umahiri katika Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu matumizi ya vionjo vya kisasa katika ushairi wa Kiswahili. Utafiti huu ulijikita katika kulinganisha na kulinganua vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahili katika diwani za Kichomi na Tungizi za Mnyagatwa. Vionjo katika tasnifu hii imetumika kama hali ya umajaribio au mwondoko wa utanzu wa ushairi au utanzu fulani kutoka sura iliyozoeleka kwenda sura mpya ambayo haijazoeleka. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni: kubainisha vionjo vya fasihi ya kisasa katika diwani teule, kufafanua sababu za matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika diwani teule na kulinganisha na kulinganua vionjo vya fasihi ya kisasa vilivyomo katika diwani teule. Mtafiti ameamua kuchunguza matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahili kwa sababu matumizi ya vionjo vya kisasa yamechunguzwa zaidi katika utanzu wa riwaya na tamthiliya, katika ushairi uchunguzi si toshelevu au havijafanyiwa uchunguzi wa kutosha. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbalimbali kama vile majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya mahojiano ili kupata data za utafiti wetu. Utafiti ulitumia nadharia ya usasa ambayo huamini katika kuanzisha vionjo vipya na kuendeleza utamaduni wa fasihi pendwa. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa utanzu wa ushairi wa Kiswahili umesheheni sana matumizi ya vionjo vya kisasa. Matumizi haya ya vionjo vya kisasa katika ushairi yanachangiwa na mambo mbalimbali kama vile mabadiliko ya kijamii, umajaribio, ongezeko la wasomi, maingiliano ya kiulimwengu, mahitaji ya hadhira na hata maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa. Mchango mpya wa tasinifu hii ni kuonesha vionjo vinavyotumiwa na waandishi mbalimbali katika utunzi hasa katika ushairi wa Kiswahili.en_US
dc.identifier.citationKalinga, J. (2020). Matumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahli: Ulinganisho wa Kichomi na Tungizi za Mnyagatwa (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/2854
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectVionjoen_US
dc.subjectUshairien_US
dc.subjectTungizi za Mnyagatwaen_US
dc.subjectDodomaen_US
dc.subjectFasihien_US
dc.subjectUshairi kiswahilien_US
dc.subjectDiwani za Kichomien_US
dc.titleMatumizi ya vionjo vya fasihi ya kisasa katika ushairi wa Kiswahli: Ulinganisho wa Kichomi na Tungizi za Mnyagatwaen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
JOYCE KALINGA.pdf
Size:
1010.66 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: