Mabadiliko katika nyimbo za taarab na uwasilishaji wake kulingana na wakati

dc.contributor.authorKhamis, Nadra Soud
dc.date.accessioned2018-10-09T06:22:02Z
dc.date.available2018-10-09T06:22:02Z
dc.date.issued2017
dc.descriptionShahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahilien_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kuchunguza mabadililko ya nyimbo za taarab na uwasilishaji wake kulingana na wakati, ambao ulifanyika katika Mkoa wa Mjini Magharib. Jambo kubwa lililozungumziwa katika utafiti huu ni kuchunguza namna ya matukio ya kihistoria katika jamii ya Zanzibar yalivyoweza kuathiri mabadiliko ya nyimbo za taarab na uwasilishaji wake katika vipindi husika. Kama inavyoeleweka kuwa, Zanzibar imepitiwa na vipindi mbalimbali kihistoria kama vile kipindi cha utawala wa Sultan, harakati za Mapinduzi na Uhuru na pia baada ya Mapnduzi hadi sasa. Kutokana na vipindi hivi ambavyo Zanzibar imepitia, moja kwa moja vimeweza kuathiri nyimbo za taarab kwa kutungwa na kuimbwa kulingana na wakati husika., hali hii imesababishwa na kuwa, fasihi maisha yote huwasawiri yaliyomo katika jamii. Kwa hali hiyo basi, hata utanzu huu wa nyimbo za taarab umeweza kuyasawiri yale yaliyomo katika jamii katika vipindi mbalimbali ambavyo nyimbo hizi zimepitia, na kusababisha kuibuka kwa nyimbo mbali mbali katika kipindi husika. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbali mbali kama vile, kusoma majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya mahojiano na majadiliano, ambapo mbinu hizi zilitusaidia katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali zilizohusu mada ya utafiti huu. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Mwigo, ambayo inahusu namna kazi za sanaa ikiwemo fasihi, zinavyoweza kuiga au kuchota yaliyomo katika jamii katika vipindi mbali mbali. Uchambuzi wa data uliegemea katika maelezo kwa kuwa utafiti huu ni wa kitaamuli.en_US
dc.identifier.citationKhamis, N. S. (2017). Mabadiliko katika nyimbo za Taarab na uwasilishaji wake kulingana na wakati. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/453
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectNyimboen_US
dc.subjectMjini Maghariben_US
dc.subjectZanzibaren_US
dc.subjectFasihien_US
dc.subjectSiti bint Saaden_US
dc.subjectJuma Shehaen_US
dc.subjectSaid Mwinyien_US
dc.subjectAbdul Alien_US
dc.subjectRukia Ramadhanen_US
dc.subjectTaaraben_US
dc.subjectMapinduzien_US
dc.subjectUngujaen_US
dc.subjectMpungaen_US
dc.subjectAfro Mamaen_US
dc.subjectHindustanien_US
dc.subjectKijitien_US
dc.subjectTanzuen_US
dc.subjectMatukioen_US
dc.subjectHistoriaen_US
dc.subjectWimboen_US
dc.subjectSultanen_US
dc.subjectUtawalaen_US
dc.titleMabadiliko katika nyimbo za taarab na uwasilishaji wake kulingana na wakatien_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
NADRA SOUD - RIPOTI.pdf
Size:
1.41 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: