Ujumi katika muziki wa dansi: mfano kutoka nyimbo teule za Marijani Rajabu na Ally Choki

dc.contributor.authorLaswai, Agripina
dc.date.accessioned2019-01-18T09:47:01Z
dc.date.available2019-01-18T09:47:01Z
dc.date.issued2015
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii ni matokeo ya utafiti uliojigeza katika kuchambua vipengele vya kiujumi katika muziki wa dansi wa wanamuziki wawili Marijani Rajabu na Ally Choki. Utafiti ulilenga kuchunguza ujumi katika muziki wa dansi wa Tanzania ili kuthibitisha kuwa taaluma ya ujumi ina nafasi kubwa katika kazi za muziki wa dansi. Pia tasnifu hii imejaribu kuona ni kwa kiasi gani, kazi hizo zenye mwelekeo wa kiujumi zinafungamana na idili za jamii ya Watanzania. Aidha imejaribu kutathimini dhima ya vipengele vya kiujumi katika fani na maudhui ya nyimbo za wanamuziki teule. Njia zilizotumika kukusanya data ni kutalii uwandani na udurusi wa kimaktaba. Uchambuzi wa data ulifanywa kwa njia ya ufafanuzi. Data zilizopatikana ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo, halikadhalika, vielelezo vilitumika kwa kiasi kidogo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Kimarx. Nadharia ya Kimarx imetoa mwongozo wa kuchunguza utamaduni na maisha ya watu weusi kwa ujumla. Matokeo ya utafiti huu yameleta mchango mpya wa kitaaluma katika Fasihi ya Kiswahili. Tasnifu imebainisha kuwa uzuri hutambuliwa kwa namna tofauti kati ya jamii moja na nyingine, na ili kuyachambua vyema masuala ya kiujumi, hutupasa kujua idili za jamii husika.Tumebainisha muktadha wa utunzi wa muziki wa dansi kwa jamii ya wakati huu wa maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia. Miongoni mwa michango ni pamoja na matumizi ya idili, adabu na utiifu na umoja katika kufafanua uzuri wa kiujumi katika muziki wa dansi. Aidha, tumetathimini dhima ya vipengele vya kiujumi katika fani na maudhui ya nyimbo teule za Marijani Rajani na Ally Choki. Dhima hizo ni kuelimisha, kuburudisha, kutambulisha jamii na kuonyesha nafasi ya mwanamke katika jamii.en_US
dc.identifier.citationLaswai, A. (2015). Ujumi katika muziki wa dansi: mfano kutoka nyimbo teule za Marijani Rajabu na Ally Choki. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/544
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectLughaen_US
dc.subjectUjumien_US
dc.subjectMuzikien_US
dc.subjectMuziki wa dansien_US
dc.subjectNyimboen_US
dc.subjectMarijani Rajabuen_US
dc.subjectAlly Chokien_US
dc.subjectNadharia ya Kimarxen_US
dc.titleUjumi katika muziki wa dansi: mfano kutoka nyimbo teule za Marijani Rajabu na Ally Chokien_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
AGRIPINA LASWAI.pdf
Size:
1.02 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: