Dhima za kisarufi na kisemantiki za viambajengo vinavyohusika katika uchanganuzi wa tungo za utendeka na utendwa

dc.contributor.authorKuyenga, Fredrick E
dc.date.accessioned2023-10-12T13:29:43Z
dc.date.available2023-10-12T13:29:43Z
dc.date.issued2022
dc.descriptionAbstract. full text article available at. . https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/4809en_US
dc.description.abstractMakala haya yamechunguza tungo za utendeka na utendwa katika lugha ya Kiswahili. Lengo ni kuweka wazi dhima za kisarufi na kisemantiki za viambajengo vinavyohusika katika tungo hizo. Hii ni kwa sababu, yapo madai miongoni mwa wanaisimu mbalimbali kwamba tungo hizi zinafanana katika miundo na uamilifu wake katika lugha kisarufi; yaani kiima katika tungo hizi kinahusishwa na kiathirika au na kithimu pekee (taz. Khamisi, 1972; Rugemalira, 1993 na Mkude, 2005). Iko haja ya kubainisha zaidi dhima za kisarufi na za kisemantiki za viambajengo vyote vinavyohusika katika tungo hizi ili kuweza wazi suala hili katika lugha ya Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka katika magazeti mawili (2) pamoja na watoataarifa kumi (10). Data zilipatikana kwa njia ya usomaji wa nyaraka pamoja na usaili. Uchanganuzi wa data umetumia misingi ya Mkabala wa Sarufi Leksia Amilifu ulioasisiwa na Bresnan na Kaplan mwishoni mwa miaka ya 1970. Matokeo yanaonesha kwamba tungo za utendeka na utendwa zinafanana na kutofautiana katika miundo na uamilifu wa viambajengo katika lugha ya Kiswahili. Kutokana na matokeo haya, inapendekezwa kwamba utafiti zaidi kama huu ufanyike katika lugha nyingine za Kibantu ambazo hazijafanyiwa utafiti ili kulinganisha na kutofautisha uamilifu wa viambajengo katika lugha ya Kiswahili na lugha nyingine. Makala haya yameweka wazi dhima za kisarufi na za kisemantiki za viambajengo vyote vinavyohusika katika tungo za utendeka na zile za utendwa katika lugha ya Kiswahili.en_US
dc.identifier.citationKuyenga, F. E. (2022). Dhima za Kisarufi na Kisemantiki za Viambajengo Vinavyohusika katika Uchanganuzi wa Tungo za Utendeka na Utendwa. Mulika Journal, 40(1).en_US
dc.identifier.otherURL: https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/4809
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/4156
dc.language.isoenen_US
dc.publisherThe University of Dar es Salaamen_US
dc.subjectUchanganuzi wa tungoen_US
dc.subjectDhima za kisarufien_US
dc.subjectViambajengoen_US
dc.subjectTungo za utendeka na utendwaen_US
dc.subjectTungoen_US
dc.subjectDhima za kisarufi na kisemantikien_US
dc.subjectUchanganuzi wa tungoen_US
dc.subjectSarufien_US
dc.subjectSarufi leksiaen_US
dc.subjectUamilifu wa viambajengoen_US
dc.titleDhima za kisarufi na kisemantiki za viambajengo vinavyohusika katika uchanganuzi wa tungo za utendeka na utendwaen_US
dc.typeArticleen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Fredrick Emanuel Kuyenga.pdf
Size:
113.27 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Main article
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections