Ufasihi katika Kasida za Madrasa
dc.contributor.author | Mganga, Nawaje Ali | |
dc.date.accessioned | 2020-03-05T07:49:03Z | |
dc.date.available | 2020-03-05T07:49:03Z | |
dc.date.issued | 2014 | |
dc.description | Tasnifu (MA Kiswahili) | en_US |
dc.description.abstract | Huu ni utafiti uliofanywa juu ya ufasihi katika kasida za madrasa kutoka wilaya ya Mjini Zanzibar kwa mwaka 2013. Tafiti mbalimbali zimefanyika kabla ya utafiti huu, lakini zote hizo zimeelezea maana ya kasida, historia na dhima ya jumla ya kasida ambayo ni kumsifu mtume Muhammad (s.a.w) mfanoSimiyu (2011:89)naMulokozi (2011:14). Dhana hiyo pia imeelezwakablana BAKIZA (2010:147),Paden (2009), Tuzin (2009),Al-Mubarakpuri (2004:310), Ntarangwi (2004:67) naMulokozi (1996:70).Kwa kuchunguza kwa undani tafiti hizi zote hazijaelezea ufasihi unaojitokeza katika kasida za madrasa. Madhumuni ya utafiti huu ni kuchunguza ufasihi unaojitokeza katika kasida za madrasa. Kama wasemavyo BAKIZA (2010:82) kuwa fasihi ni sanaa ya lugha. Hivyo usanii wa kasida ni mbinu mbali mbali zilizotumika katika kasida za madrasa zenye kudhihirisha ufundi au usaniiwa lugha. Kwa mfano matumizi ya lugha, ujenzi wa muundo, uteuzi wa mtindo na uibuaji wa dhamira. Utafiti huu ni muhimu katika taaluma ya fasihi simulizi hasa katika vipengele vya fani na maudhui pamoja na kubainisha utendaji wa kasida za madrasa za wilaya ya Mjini Zanzibar.Utafiti huu utawafaa wanazuoni wengine wanaotaka kufanya utafiti zaidi kuhusu kasida. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa kianzio kwa yale masuala ambayo hajashughulikiwa katika utafiti huu. Mbinu shirikishi (kuangalia), mahojiano ya ana kwa ana na dodoso la maswali zilitumika katika kukusanya data za utafiti huu. Hatimaye nadharia ya Ujumi wa Kinudhuma ilitumika wakati wa kuwasilisha na kufafanua data za utafiti huu. | en_US |
dc.identifier.citation | Mganga, N. A. (2014). Ufasihi katika Kasida za Madrasa (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma. | en_US |
dc.identifier.uri | http://hdl.handle.net/20.500.12661/1996 | |
dc.language.iso | Kisw | en_US |
dc.publisher | Chuo Kikuu cha Dodoma | en_US |
dc.subject | Madrasa | en_US |
dc.subject | Kasida | en_US |
dc.subject | Ufasihi | en_US |
dc.subject | Dini | en_US |
dc.subject | Zanzibar | en_US |
dc.subject | Fasihi simulizi | en_US |
dc.subject | Ujumi | en_US |
dc.subject | Nudhuma | en_US |
dc.subject | Watoto | en_US |
dc.title | Ufasihi katika Kasida za Madrasa | en_US |
dc.type | Dissertation | en_US |