Wahusika wa kimimi katika riwaya ya Kiswahili: mifano kutoka dunia yao na nyuso za mwanamke

Loading...
Thumbnail Image
Date
2018
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Utafuti huu ulilenga kuchunguza wahusika wa Kimimi katika riwaya za Said Ahmed Mohamed kwa kujikita katika miktadha ya utokeaji wa wahusika hao, namna wahusika wanavyojikengeusha na jamii; na sababu za wahusika kujikengeusha. Matumizi ya wahusika wa Kimimi hayajachunguzwa vya kutosha. Yumkini, hali hii inasababisha kutokufahamika miongoni mwa wasomaji na wahakiki wa kazi za fasihi. Kazi tulizozipigia mbizi kwa kina katika kuchunguza wahusika wa Kimimi ni riwaya ya Dunia Yao na Nyuso za Mwanamke. Utafiti ulifanyika maktabani. Maeneo yaliyotumika kukusanyia data ni Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Zanzibar. Hakuna data yoyote ya kitakwimu iliyotumika katika utafiti huu, bali tulitumia mbinu ya ufafanuzi. Uchambuzi wa data umefanyika kwa kutumia mkabala wa kisaikochanganuzi ambapo uchambuzi ulifanyika kwa mbinu ya ufafanuzi. Matokeo yanaonesha kuwa, riwaya ya Dunia Yao na Nyuso za Mwanamke zimetumia miktadha ya chimbuko la kifasihi, kisiasa, shereheni, kazini, kifamilia, mahakamani na mitaani.Pia, wahusika wamejikengeusha kwa kugomea chakula, kutojali, ukivuli, kutokata tamaa, kushiriki ngono, usasa, ulevi na uongozi bora. Sababu za wahusika kujikengeusha ni ukosefu wa ajira, utandawazi, ukombozi wa mwanamke, siasa, utamaduni, habari na mawasiliano na usomi. Utafiti uliongozwa na mkabala wa Saikochanganuzi.Mchango mpya ulioibuliwa na utafiti huu katika taaluma ya fasihi ni huu. Mosi, kuibuliwa kwa miktadha ambayo wahusika wa Kimimi wamesawiriwa katika riwaya ya Dunia Yao na Nyuso za Mwanamke. Pili, Kufafanuliwa sababu za wahusika kujikengeusha na jamii. Tatu, kuibuliwa kwa sababu za wahusika kujikengeusha ambazo ni ukombozi, siasa, utamaduni na usomi.
Description
Tasnifu (Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili)
Keywords
Kimimi, Nyuso, Mwanamke, Dunia, Fasihi, Tamaa, Usasa, Ulevi, Ajira, Ukombozi, Maadili
Citation
Ali, H. B. (2018). Wahusika wa kimimi katika riwaya ya Kiswahili: mifano kutoka dunia yao na nyuso za mwanamke (Tasnifu shahada ya umahiri). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.