Mabadiliko ya vionjo vya kiuandishi katika riwaya ya Kiswahili: Ulinganisho wa riwaya za Shaaban Robert na Said A. Mohamed

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Tasnifu hii inahusu Mabadiliko ya Vionjo vya Kiuandishi katika Riwaya ya Kiswahili. Utafiti ulijigeza katika kulinganisha na kulinganua mabadiliko hayo katika riwaya za Shaaban Robert na Said A. Mohamed. Neno vionjo katika tasnifu hii limetumika kama hali ya kimajaribio au mwondoko wa utanzu fulani wa Fasihi kutoka sura iliyozoeleka kwenda sura mpya ambayo haijazoeleka. Mtafiti ameamua kuchunguza mabadiliko ya vionjo vya kiuandishi katika riwaya ya Kiswahili kwa sababu, kwa kiasi kikubwa bado dhana hii ya mabadiliko ya vionjo vya kiuandishi haijafanyiwa uchunguzi. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbalimbali kama vile majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya mahojiano ili kupata data za utafiti wetu. Utafiti ulitumia nadharia ya uhalisia ambayo humtaka mtunzi kutunga kwa kuzingatia suala la wakati pamoja na kujua historia ya jamii husika. Mabadiliko haya katika riwaya ya Kiswahili yanazingatia pia vitu hivyo. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa uandishi wa riwaya ya Kiswahili umebeba mabadiliko kadhaa katika uandishi wake. Mabadiliko haya katika vionjo vya kiuandishi yanachangiwa sana na vitu kama vile mabadiliko ya kijamii (historia za jamii), umajaribio, ongezeko la wasomi na hata maendeleo ya sayansi na tekinolojia kwa kiasi kikubwa. Mchango mpya wa tasnifu hii ni kuonesha vionjo vinavyotumiwa na waandishi mbalimbali katika utunzi hasa katika riwaya ya Kiswahili.
Description
Tasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
Keywords
Kiswahili, Riwaya, Utanzu, Uandishi, Mabadiliko, Durusu, Uwandani, Sayansi, Tekinolojia, Ulinganisho, Swahili, Utunzi, Sayansi na Tekinolojia, Vionjo vya Kiuandishi, Shaaban Robert, Said A. Mohamed, Fasihi andishi
Citation
Jumanne, A. (2016). Mabadiliko ya vionjo vya kiuandishi katika riwaya ya Kiswahili: Ulinganisho wa riwaya za Shaaban Robert na Said A. Mohamed (Tasnifu shahada ya uzamili). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.