Athari za sayansi na teknolojia katika hadithi za watoto: mifano ya ngano kutoka wilaya ya Micheweni Pemba

dc.contributor.authorMbarouk, Mbarouk Juma
dc.date.accessioned2019-08-21T09:23:01Z
dc.date.available2019-08-21T09:23:01Z
dc.date.issued2015
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza hadithi za watoto, kwa kuangalia jinsi hadithi hizo zilivyoathiriwa na maendeleo ya sasa ya sayansi na teknolojia. Hususan, kwa kuchunguza mifano ya hadithi za ngano kutoka Wilaya ya Micheweni Zanzibar. Utafiti ulibaini kwamba, sifa nyingi za Fasihi Simulizi zimebadilika au zimo katika mabadiliko makubwa. Hasa hasa katika kipindi hiki cha kukua na kuimarika kwa sayansi na teknolojia. Ikiwa hivyo ndivyo, basi ni dhahiri kwamba Fasihi Simulizi na vipera vyake inafaa vizidi kuchunguzwa zaidi, ili kujua ni kwa namna gani vipera hivyo vimeathiriwa na maendeleo hayo ya sayansi na teknolojia. Utafiti huu umeongozwa na malengo matatu, ambayo ni kuchunguza madhara yanayotokana na sayansi na teknolojia jinsi yanavyoathiri usimuliaji na uhifadhi wa hadithi za watoto, hususan hadithi za ngano, kutathmini mchango wa sayansi na teknolojia katika maendeleo ya utanzu wa hadithi za watoto, kwa kuangalia mifano ya ngano kutoka Wilaya ya Micheweni Zanzibar na lengo la tatu ni kuchunguza mwamko wa wanajamii wa Wilaya ya Micheweni walioupata kuhusiana na athari ya sayansi na teknolojia katika utanzu wa hadithi za watoto, kwenye mifano ya hadithi za ngano. Katika malengo matatu hayo kila lengo lilipewa nafasi kutegemea na matokeo ya utafiti wenyewe. Katika tasnifu hii, mkabala uliotumika ni wa nadharia ya Uhalisia. Nadharia hii imekuwa na umuhimu mkubwa sana katika kupata matokeo bora ya utafiti huu. Kwani nadharia hii ya uhalisia imetusaidia katika kujiridhisha kwamba, kila lengo tulilolijadili linasawiri uhalisi uliopo katika jamii ambayo ililengwa kufanyiwa utafiti. Matokeo ya utafiti huu ni kwamba, utatoa mchango mkubwa katika uga huu wa Fasihi Simulizi kwani ni sehemu muhimu ya chanzo cha taarifa za kifasihi. Utafiti huu unategemewa pia kuwa na faida kubwa kwa taifa, kwani utasaidia kufafanua hadithi za watoto, kwa kuangalia mifano ya ngano ambazo, kwa kiasi fulani, zinaelekea kupotea kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Pia utasaidia kuzifanya hadithi hizo zisambae na kufahamika na watu wengi ndani na nje ya nchi yetu.en_US
dc.identifier.citationMbarouk, M. J., (2015). Athari za sayansi na teknolojia katika hadithi za watoto: mifano ya ngano kutoka wilaya ya Micheweni Pemba. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1047
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectAtharien_US
dc.subjectAthari za sayansien_US
dc.subjectAthari za teknolojiaen_US
dc.subjectHadithien_US
dc.subjectNganoen_US
dc.subjectMichewanien_US
dc.subjectPembaen_US
dc.subjectTeknolojiaen_US
dc.subjectHadithi za watotoen_US
dc.titleAthari za sayansi na teknolojia katika hadithi za watoto: mifano ya ngano kutoka wilaya ya Micheweni Pembaen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
MBAROUK JUMA MBAROUK.pdf
Size:
1.48 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: