Korasi katika tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyoni

dc.contributor.authorKiloba, Leah Yusufu
dc.date.accessioned2020-03-05T07:46:03Z
dc.date.available2020-03-05T07:46:03Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulihusu Korasi katika Tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyoni. Dhana ya korasi imetumiwa ikimaanisha matendo, fikra au maneno ya kisanaa ayatoayo mtu au kikundi cha watu katika kitendo cha kisanaa kwa njia ya uimbaji, uradidi, nathari na kuambatana na vitendo. Matumizi ya mbinu hii ya korasi hayajatafitiwa wala kuhakikiwa vya kutosha katika Fasihi ya Kiswahili. Hali hii inakifanya kipengele hiki kutojulikana sana na wasomi na wanajamii wengi. Tamthiliya za waandishi teule zilizotafitiwa ni Kwenye Ukingo wa Thim, Ngoma ya Ng’wanamalundi na Mabepari wa Bongo. Utafiti huu ulifanyika maktabani kwa kiasi kikubwa. Vilevile mtafiti alifanikiwa kuzungumza na wataalamu mbalimbali wa fasihi ili kupata mawazo komavu kuhusiana na mada. Uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti uliongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji kupitia nguzo yake kuu ya uhuru wa msomaji wa kupata maana kutokana na uzoefu wake. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kipengele cha korasi hutumika katika tamthiliya kwa malengo mahususi na wala si kwa bahati nasibu tu. Mchango mpya ulioibuliwa na utafiti huu ni: Kwanza, ni kupanua ufafanuzi wa dhana ya korasi. Pili, ni kuonyesha nafasi ya korasi katika tamthiliya, hususani katika tamthiliya za waandishi teule. Tatu, ubainishaji na uchambuzi wa dhima za korasi ambazo ni kutambulisha onyesho, kuunganisha onyesho moja na jingine, kuwasilisha dhamira, kudhihirisha ujumi, kujenga taharuki, kuleta ucheshi na kufunga onyesho. Hivyo, korasi hutumika kama nguzo katika ujenzi na uendelezaji wa tamthiliya.en_US
dc.identifier.citationKiloba, L. Y. (2014). Korasi katika tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyoni (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1993
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectKorasien_US
dc.subjectTamthiliyaen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectUimbajien_US
dc.subjectUradidien_US
dc.subjectTamthiliya kiswahilien_US
dc.subjectDhimaen_US
dc.subjectKwenye ukingo wa Thimen_US
dc.subjectNadharia mwitikoen_US
dc.subjectEbrahim Husseinen_US
dc.subjectEmmanuel Mbogoen_US
dc.subjectFrowin Nyonien_US
dc.subjectNgoma Ng’wanamalundien_US
dc.subjectMabepari bongoen_US
dc.titleKorasi katika tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyonien_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Leah Kiloba.pdf
Size:
870.12 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: