Athari za maendeleo ya sayansi na teknolojia kwenye nyimbo za asili za Wapare

dc.contributor.authorAzizi, Ally
dc.date.accessioned2020-03-05T05:26:16Z
dc.date.available2020-03-05T05:26:16Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)en_US
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza Athari za Maendeleo ya Sayansi na Teknoilojia kwenye Nyimbo za Asili za Wapare. Mtafiti alichochewa naukweli kwamba hata kama waandishi wa fasihi simulizi, hasa nyimbo za makabilaya Kitanzania,walikuwa wamefanya kazi kubwa ya kuchambua nyimbo hizo kwa namna mbalimbali, lakini hawakuangalia na kujali uchambuzi na uchanganuzi wa athari za sayansi na teknolojia kwenye nyimbo za asili za Wapare. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Sosholojia katika uchambuzi wa data za utafiti. Msingi wa nadharia hii inaangalia uhusiano uliopo baina ya fasihi na jamii na kwamba, mabadiliko yanayotokea katika jamii ndiyo yanayosababisha kubadilika kwa fasihi na nyimbo za asili zikiwemo. Mbinu mbalimbali zilizotumika kwenye ukusanyaji wa data za utafiti huu ni usaili na ushuhudiaji, pamoja na ushiriki katika kukusanya data. Baada ya uchambuzi wa data utafiti huu uliweza kubaini kuwa, maendeleo ya sayansi na teknolojia yana athari chanya na hasi kwenye nyimbo hizo za asili za Wapare. Utafiti huu umegundua kwamba ni vigumu kuchagua faida tu za maendeleo ya sayansi na teknolojia bila ya kupata hasara zake. Utafiti ulionapia jamii ndiyo yenye jukumu la kuchagua kipi kiwepo na kipi kisiwepo katika mfumo wa maisha ya jamii husika kulingana na msukumo wa mabadiliko katika jamii. Ukweli ni kwamba hakuna chenye faida kisicho na hasara zake kwa namna yoyote ile. Utafiti huu unapendekeza kwamba ipo haja ya tafiti mbalimbali kufanyika kuhusu athari za maendeleo ya sayansi na teknolojia kwenye tanzu zingine za fasihi kama vile methali, vitendawili, na sanaa za maonyesho ili kuweza kubaini ni kwa namna gani maendeleo ya sayansi na teknolojia yameweza kuiathiri fasihi simulizi kwa undani zaidi.en_US
dc.identifier.citationAzizi, A. (2014). Athari za maendeleo ya sayansi na teknolojia kwenye nyimbo za asili za Wapare (Tasnifu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1979
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectSayansien_US
dc.subjectTeknolojiaen_US
dc.subjectWapareen_US
dc.subjectFasihien_US
dc.subjectFasihi simulizien_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.subjectNyimbo asilien_US
dc.subjectJamii wapareen_US
dc.subjectAthari maendeleoen_US
dc.subjectNyimbo makabilaen_US
dc.subjectNyimbo wapareen_US
dc.titleAthari za maendeleo ya sayansi na teknolojia kwenye nyimbo za asili za Wapareen_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Azizi Ally.pdf
Size:
1.89 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: