Athari za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa nyimbo za watoto waishio Mijini

dc.contributor.authorHemed, Bimkubwa Abdulrahman
dc.date.accessioned2019-08-20T08:29:34Z
dc.date.available2019-08-20T08:29:34Z
dc.date.issued2015
dc.descriptionTasnifu ( Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umechunguza namna Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inavyoathiri nyimbo za watoto hususan maeneo ya mijini ambako maendeleo hayo ya sayansi na teknolojia ndiko yanakopatikana kwa wingi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Usosholojia iliyoasisiwa kwa kuja kupingana na ulimbwende karne ya kumi na tisa. Utafiti huu umejumuisha mbinu ya mahojiano na hojaji kukusanya data hatimaye imechanganuliwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano yaliyopo nchini hususan mijini, yameathiri kwa kiasi kikubwa nyimbo za watoto kutokana na kuwepo kwa vyombo vingi vya habari hapa nchini, ambao ushindani wao wa kibiashara ndio unaowafanya warushe hewani nyimbo za wasanii mbali mbali na kuacha zile za watoto ambapo watoto walikuwa wanaziimba kabla yake. Suala la msingi lililobainishwa na utafiti huu ni kwamba nyimbo za watoto zimeathiriwa na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mapendekezo yafuatayo yamezingatiwa. Serikali na jamii wafanye juhudi za makusudi kurejesha hadhi ya nyimbo za watoto kwa kuziingiza katika mitaala ya shule pamoja na wazazi kufanya juhudi za makusudi kuwafundisha nyimbo hizo ili zisiendelee kupotea. Pia, imependekezwa tafiti zaidi zifanywe kuhusu tanzu mbalimbali za fasihi simulizi, na kwamba watafiti wasikidharau kipengele hiki cha nyimbo za watoto kwani mbali na kutoa burudani, pia watoto hupata mazoezi ya kutosha nakuwafanya wawe wakakamavu na wenye afya.en_US
dc.identifier.citationHemed, B. A. (2015). Athari za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa nyimbo za watoto waishio Mijini. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/987
dc.language.isoKiswen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodomaen_US
dc.subjectTeknolojia ya habari na mawasilianoen_US
dc.subjectTEHAMAen_US
dc.subjectNyimboen_US
dc.subjectNyimbo za watotoen_US
dc.subjectMijinien_US
dc.subjectUsosholojiaen_US
dc.titleAthari za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa nyimbo za watoto waishio Mijinien_US
dc.typeDissertationen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
BIMKUBWA ABDULRAHMAN HEMED.pdf
Size:
1.31 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: