Master Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Master Dissertations by Author "Bayyo, Festo Banga"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Usawiri wa jinsi ya kiume katika riwaya teule za Shafi Adam Shafi(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2020) Bayyo, Festo BangaTasinifu hii inahusiana na usawiri wa jinsi ya kiume katika riwaya teule za Shafi Adam Shafi. Tasinifu hii imejengwa na malengo matatu yafuatayo: kubainisha namna jinsi ya kiume ilivyosawiriwa katika riwaya za Shafi Adam Shafi. Pia, kubainisha changamoto zinazoikabili jinsi ya kiume katika riwaya za Shafi Adam Shafi. Lengo la tatu, ni kuelezea mbinu zilizotumiwa na jinsi ya kiume katika kukabiliana na changamoto hizo. Matokeo ya utafiti uliofanyika yametolewa kwa kuzingatia malengo na maswali ya utafiti kwa kuongozwa na nadharia ya uhalisia. Kuhusu lengo la kwanza, utafiti umebaini kuwa, jinsi ya kiume inasawiriwa kama jinsi yenye ujasiri, uvumilivu, msimamo, uongozi, wanamapinduzi na katili. Kuhusu lengo la pili, utafiti umebaini kuwa, umebainisha changamoto kama: kukosa elimu, hali ngumu ya maisha, usaliti, kukosa haki na kutenganishwa na familia. Kuhusu lengo la tatu, utafiti umebaini kuwa, mbinu kama: kutafuta burudani, kushirikiana, kudai haki zao (migomo) na kutoroka shida; ni baadhi ya mbinu zinazotumiwa na jinsi ya kiume kukabiliana na changamoto husika. Kukamilika kwa tasinifu hii kumetoa mchango mpya katika uwanja wa fasihi ya Kiswahili. Kwanza, kuipa jinsi ya kiume nafasi ya kutazamwa kama ambavyo jinsi ya kike inatazamwa. Pia, kubainisha changamoto zinazoikabili jinsi ya kiume katika kuhakikisha wanafikia malengo yao. Tatu, tasinifu hii imetoa mwanga katika masuala yanayohusiana na masuala ya jinsi katika fasihi ya Kiswahili.