Master Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Master Dissertations by Subject "Amali"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Dhima ya visasili katika kuhifadhi na kurithisha amali za kitamaduni: mifano kutoka kwa Wasukuma(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2014) Mgunda, John MadirishaVisasili ni hadithi zinazoelezea desturi, itikadi, jadi na dini ambazo watu wa kale walizifuata (kuzishika) kutokana na mafundisho yaliyotokana na masimulizi hayo, wakiwa na uwezo wa kufanya miujiza kutokana nguvu za asili. Visasili vina dhima ya kuelimisha, kuonya, kuburudisha na kuadilisha kama tanzu zingine za fasihi simulizi. Utafiti huu ulikusanya visasili na kuchambua amali za kitamaduni za jamii ya Wasukuma ambazo zinahifadhiwa na kurithishwa katika visasili hivyo. Katika kukidhi matakwa ya malengo ya utafiti huu, kiunzi cha nadharia ya Masimulizi ya Mdomo na Uasilia zilitumiwa katika kuchambua data. Data zilikusanywa katika wilaya ya Magu, Kwimba, Nyamagana na Misungwi. Mbinu ya hojaji ilitumika sambamba na maandiko mbalimbali kutoka kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dodoma na Dar es Salaam, maandiko yaliyotafiti kuhusu visasili vya jamii mbalimbali, vilevile, katika kupata wawakilishi utafiti huu ulitumia sampuli lengwa (ya kimakusudi) kwa kuzingatia sifa za watafitiwa. Utafiti huu umebaini kuwa, uhifadhi na urithishaji wa fasihi simulizi katika jamii, utaisaidia kutunza kumbukumbu za asili za jamii ya Wasukuma, kuwasaidia watafiti katika utanzu huu wa visasili na kupanua mawanda mapana ya uelewa katika jamii. Visasili kama tanzu zingine za fasihi simulizi, huonesha asili ya jamii husika hasa kupitia kwenye masimulizi na matambiko. Ni utanzu unaorejesha fikra za mwanadamu kuona namna wanadamu wa kale walivyoishi kwa kuabudu miungu waliyoiamini na kuwatatulia matatizo yao. Hakuna jamii ambayo haina historia yake na utamaduni wake, hivyo, wataalam mbalimbali wa fasihi simulizi wanapaswa kushughulika katika tafiti mbalimbali ili kupata ukweli wa kila jamii wa desturi na mila zake.Item Ontolojia ya kiafrika katika mbolezi za wanyasa(Chuo Kikuu cha Dodoma, 2018) Kaponda, George JohnTasnifu hii inahusu Ontolojia ya Kiafrika katika Mbolezi za Wanyasa. Utafiti huu ulifanywa uwandani na maktabani ambapo uwandani, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, ushuhudiaji na mjadala wa vikundi. Kwa upande wa maktabani mtafiti alitumia mbinu ya udurusu maktaba.Utafiti uliongozwa na lengo kuu ambalo ni kubaini vipengele vya ontolojia ya Kiafrika katika mbolezi za Wanyasa. Malengo mahususi ambayo ni; kubainisha aina ya mbolezi zinazopatikana katika jamii ya Wanyasa, kubainisha vipengele vya ontolojia ya Kiafrika ya katika mbolezi za Wanyasa na kutathimini umuhimu wa ontolojia ya Kiafrika kwa jamii ya Wanyasa na Waafrika kwa ujumla. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Ontolojia, mtafiti alikusanya mbolezi na dhana mbalimbali za ontolojia ya Kiafrika katika jamii ya Wanyasa. Jumla ya watafitiwa walioshiriki ni mia moja. Katika data zilizokusanywa, vipengele vilivyojitokeza vilijenga msingi wa data kuu iliyofanyiwa uchambuzi na kujadiliwa. Matokeo yanaonesha kuwa mbolezi zimegawanyika kulingana na vigezo vya chimbuko, rika na wakati. Katika chimbuko kuna mbolezi za asili na mbolezi changamani. Katika rika kuna mbolezi za watoto na mbolezi za watu wazima. Aidha, katika wakati kuna mbolezi za mara baada ya msiba kutokea, buriani, ibada ya mazishi na mazishi. Vipengele vya ontolojia ya Kiafrika vilivyobainishwa ni Mungu, ardhi, roho, kifo, mizimu na utu. Vipengele hivi vimebainika kuwa vimejengwa kiherakia na kutegemeana katika nguvu ijulikanayo kama kani uhai. Aidha, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa jamii inaendelea kudumisha umoja na mshikamano, kurithisha amali, kulinda maadili, kutolea elimu na utambulisho wa jamii. Utafiti huu umependekeza tafiti nyingi zaidi ziendelee kufanyika kuhusiana na ontolojia ya Kiafrika katika fasihi simulizi.